Header Ads


MBUNGE WA MBOZI KUPITIA CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO CHADEMA PASCAL HAONGA AMEWATAKA WANANCHI WA WILAYA HIYO KUCHOMA NYUMBA YAKE ENDAPO ATAHAMIA CCM







Mbozi
MBUNGE wa Jimbo la Mbozi mkoani Songwe, (Chadema), Pascal Haonga, amewataka wananchi mkoani hapa kuendelea kumuunga mkono katika shughuli za maendeleo huku akiahidi kuwa hawezi kuwasaliti wananchi wake kwa kuhama chama hicho.
Haonga ameahidi kubaki ndani ya chama hicho siku zote huku akiendelea kusimamia shughuli za maendeleo na kuwataka wananchi kuchoma nyumba yake iwapo atahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Haonga ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipowahutubia wananchi wa Mji wa Mlowo wilayani Mbozi, ambapo amesema hawezi kuwasaliti wananchi waliosimama kidete kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuhakikisha anapata ushindi ambapo amesema kulikuwa na matukio ya vurugu katika jimbo hilo huku baadhi ya watu wakipoteza biashara zao, kujeruhiwa hivyo hawezi kuwasailiti.

Aidha, katika mkutani huo haonga alisoma mapato na matumizi ya mfuko wa jimbo na kwamba anaendelea kuzitumia fedha hizo kwaajili ya kuboresha miundombinu zikiwamo zahanati, vyumba vya madarasa kwenye shule za msingi na sekondari pamoja na barabara ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kuchangia.

Idadi kubwa ya madiwani wa upinzani wamejiuzulu na kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM wakati wabunge watatu hadi sasa wamejiuzulu na kuhama vyama vyao ambao ni Godwin Mollel (Siha-Chadema) aliyehamia CCM, Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini-CCM) aliyehamia Chadema na Maulid Mtulia (Kinondoni-CUF) aliyejiuzulu na kujiunga na CCM.

No comments

Powered by Blogger.