WASAMBAZAJI WA MBOLEA WILAYANI KYYELA MKOANI MBEYA WAMEPEWA ONYO NA MKUU WA WILAYA HIYO CLAUDIA KITTA KUFUTATA TARATIBU ZA SERIKALI ZAKUUZA KWA BEI ELEKEZI
Mbeya
MKUU wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya,Claudia Kitta,amewataka
wafanyabiashara waliopewa tenda ya kuuza mbolea kwa bei elekezi kuuza kwa
kufuata utaratibu uliowekwa wa kuuza kwa bei elekezi badala ya kupandisha bei
inayomnyonya mkulima.
Serikali imebadiri mfumo wa ugawaji
pembejeo kwa mtindo wa vocha baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi ya wakulima
kuwa hawanufaiki na mfumo huo ambapo mwaka huu wafanyabiashara watauza kwa bei
elekezi ili kila mkulima anunue dukani.
Kufuatia mpango huo, baadhi ya
wafanyabiashara walio orodheshwa majina na kampuni zao na kupewa utaratibu huo,
wengi wao wamejiondoa kwa madai kuwa mpngo huo unawaminya na kwamba kwa
waliokubali wamepewa onyo kali baada ya kuwepo tetesi za kuuza pembejeo kwa bei
juu.
Akizungumza kwenye mdaharo
uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Biashara K.P.C. ulioitishwa na shirika la
kiraia la Jitambue Lembuka Tanzania (J.L.T) mwenyekiti wa kamati ya pembejeo
wilayani humo,Claudia Kitta,alisema ili kuhakikisha wakulima wanalima kwa
manufaa ni lazima maafisa ugani wawafuate wakulima.
Kitta ambaye pia ni mkuu wa wilaya
hiyo,amesema ikibainika wafanyabiashara wanauza pembejeo kwa bei ya kilanguzi
hata sita kuwachukulia hatua huku akieleza kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya
viwanda,ili viwanda viweze kuendelea ni lazima wakulima wazarishe mazao mengi.
Aidha Kitta alisema mbali na mkulima
kulima mazao mengi,pia aliwataka maafisa kilimo kutokaa maofisini na badala
yake waende mashambani kutoa elimu na ushauri kwa wakulima namna ya kulima
kilimo cha kisasa vinginevyo alisema hata wafumbia macho kuwawajibisha endapo
hawatafuata agizo hilo.
Post a Comment