VIJIJI VYA CHITETE NA TINDINGOMA WILAYANI MOMBA MKOANI SONGWE WATANUFAIKA NA MAJI MWAKA HUU 2018 BAADA YA KUPATA SHIDA YA MAJI MUDA MREFU
MOMBA
Zaidi ya wananchi elfu kumi
wa vijiji vya chitete na tindingoma wilaya ya momba mkoani songwe watanufaika
na miradi ya maji iliyojengwa katika maeneo hayo ambapo kuanzia wiki ijayo maji
hayo yatasambazwa na kuanza kutumiwa na wananchi hao.
Miradi hiyo ya maji ni moja kati ya miradi
inayoendelea kujengwa katika wilaya hiyo ambapo imegharimu kiasi cha shilingi
mil 900 huku uchimbaji wa visima nane vya maji katika maeneo mbali mbali
wilayani hapo ukiendelea ambapo kati ya hivyo vitatu vimechimbwa .
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya
ya momba mkoani hapa Adriani Njungu wakati wa ziara ya naibu waziri wa maji
jumaa aweso ambapo waziri huyo ametembelea miradi hiyo ikiwa ni pamoja na mradi
mkubwa unaotazamiwa kujengwa ujuliakanao kama Momba Water Siprese Skim ambao
utahudumia wakazi elf 66 katika wilaya hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya
wilaya hiyo methew chikoti ameshukuru ujio wa naibu waziri wa maji ambapo
amesema matatizo waliyokuwa wakikabiliana nayo yatakwisha kwa kukosa mwakilishi
ambapo ametumia nafasi hiyo kumuomba naibu waziri kuwapatia vitendea kazi ikiwa
ni pamoja na magari kwani yaliyopo ni mabovu.
Naye mkuu wa wilaya ya momba Juma Saidi Irando licha
ya kukiri uhitaji mkubwa wa maji katika wilaya yake amesema kukamilika kwa
mradi huo mkubwa kutasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji ambapo ametoa
rai kwa mkandarasi atakayeanza kufanya shughuli hiyo, kufanya kwa mujibu wa
sheria kwani itakapobainika mradi huo umejengwa chini ya kiwango atachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Naibu waziri wa maji jumaa aweso ameridhika na
uendeshaji wa miradi hiyo ikiwa ni pamoja na huo mradi mkubwa ambapo amemuagiza
mkandarasi anayehusika kumaliza zoezi hilo mapema kwani tayari fedha zote
zimetolewa huku akiwasihi wananchi kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo ya
maji ili waendelee kunufaika zaidi na uwepo wa maji.
Post a Comment