WAOMBA KUBOROSHEWA HUDUMA ZA AFYA WILAYA KYELA MKOANI MBEYA
MBEYA
WADAU
wa afya wilayani Kyela mkoani mkoani Mbeya wamempa changamoto mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi wilayani humo,Ally Mlaghila kuhakikisha anaondoa matatizo
ya ubovu wa huduma za matibabu na ukosefu wa vifaa tiba katika hospitali ya
wilaya hiyo.
Hospitali ya
wilaya ya Kyela ni moja ya hospitali za wilaya mkoani Mbeya ambayo licha ya
ukongwe wake imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya watu kuwa haina huduma bora
hali inayopelekea baadhi ya watu kukimbilia kwenye hospitali za wilaya ya
Rungwe yaani makandana na Igongwe kutibiwa.
Kufuatia hali
hiyo wadau mbalimbali walikutana na kujadili masuala mbalimbali
yanayohusu wilaya hiyo ikiwemo changamoto ya huduma za afya kwenye hospitali ya
wilaya baada ya uongozi mpya wa ccm kuzidi kuwashirikisha wadau kupitia vikao
kujua changamoto zilizopo na namna ya kuzitatua.
Sala Kisole
mkazi wa Kyela,kupitia kikao hicho,alisema kwa muda mrefu kumekuwepo na
malalamiko ya huduma mbovu ambapo watu wamekuwa wakikimbilia hospitali za mbali
na kuwa anapata wasiwasi kuwa hospitali ya Rungwe na Kyela zote zinahadhi
moja,kitendo cha kukimbilia Rungwe ni aibu.
Abiniuty
Mwakilewa,alisema endapo wanaKyela wataungana pamoja na kuwa kitu kimoja
wakijadili namna ya kuleta maendeleo na kuondoa changamoto zilizopo anauhakika
hakuta kuwa na malalamiko na kwamba na kuwa kitendo cha watu kukimbilia Rungwe
kupata tiba ni tatizo kubwa.
Akizungumzia
hali hiyo,Mwenyekiti wa ccm wilayani humo,Ally Mlaghila ,alisema anafahamu
kuhusu changamoto hizo na kuwa aligombea nafasi hiyo ili aweze kuisimamia
serikali kutimiza ilani kwa sababu ilani ya ccm inataka kila kijiji kiwe na
Zahanati,kata kituo cha afya na wilaya hospitali.
Alisema kwa
sasa bado vijiji vingi havina zahanati,kata nyingi hazina vituo vya afya hivyo
atahakikisha anawashirikisha wadau kuhakikisha mambo yote yaliyomo kwenye ilani
yanatekelezwa ikiwemo kufanya maboresho katika hospitali ya wilaya.
Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo,Dkt,Hunter mwakifuna simu juu ya kutatua changamoto hizo,alisema
tayari wameboresha mambo kadhaa na hata hivyo alisema serikali kwa kuona
umuhimu nwa afya wamewapa milioni 500 kujenga majengo mapya kwenye kituo cha
afya Ipinda.
Post a Comment