MCHUNGAJI AACHA KAZI HIYO YA UTUME NA KUSIMIKWA KAMA CHIEF WA KABILA LA WAMAMBWE
RUKWA
WACHUNGAJI wa kanisa la Moravian
katika jimbo la kalambo mkoani
Rukwa wamelaani vikali kitendo cha mchungajimwenzao
Sikazwe Maiko kubadiri kazi yake ya
uchungaji na kusimikwa lasimi kuwa
chifu wa
kabila la kimambwe
mwambao wa ziwa Tanganyika kinyume na madili
ya kanisa hilo.
Mchungaji
huyo alikuwa akihudumu katika kanisa
la Moravian kasanga mwambao wa ziwa
Tanganyika , ambapo siku za hivi karibuni
aliamua kubadili mwelekeo na kujiunga na
jumuhiya mafumu yaani wasaidizi wa
machifu kutoka maeneo tofauti mkoani hapa
na wa nchi za ya Zambia.
Kufuatia
hali hiyo mchungaji huyo alishawishiwa
kupatiwa cheo hicho na kuwa
kiongozi mkuu wa mila hali ambayo iliibua
tafrani kubwa kwa waumini wa
makanisa hayo pamoja na wachungaji
kwa ujumla.
Baadhi
ya wachungaji wa kanisa hilo
wamesema kitendo cha kiongozi
mwenzao kuacha kazi ya mungu na
kujiunga na uchifu ni kosa kubwa
mbele za mwenyezi mungu na kuomba
uongozi wa makanisa hayo kumvua wadhifa
wake haraka.
Mkuu
wa jimbo hilo mchungaji Simaye
Elodi Lupia ,amekiri wazi kuwepo kwa adha
hiyo na kusema wamemwandikia barua
ya kumwachisha kazi ya uchungaji.
Kwa upande wake
mchungaji huyo ambae kwa sasa ni
chifu Sikazwe Maiko, amesema ameamua kufanya
hivyo ili kundeleza mila na desturi ambazo
zimekuwa zkiipuuzwa kutokana na imani potofu.
Post a Comment