TANZANIA IMEUNGANA NA MATAIFA YA AFRIKA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA AMBAYO KILA MWAKA HUFANYIKA JUNI 16 KILA MWAKA ,AMBAYO MKOA WA SONGWE YAMEFANYIKA WILAYANI MOMBA MKOA WA SONGWE
MOMBA -SONGWE
Na.Manuel Kaminyoge
Tanzania imeungana na mataifa huru ya afrika kuadhimisha siku ya mtoto wa afrika ambayo kila mwaka hufanyika juni 16 ambayo kimkoa yamefanyika katika kijiji na tarafa ya kamsamba wilayani momba na mgeni rasimi akiwa mkuu wa mkoa wa songwe chiku galawa .
Galawa amewataka wazazi na walezi mkoani songwe kuacha maramoja tabia ya kuwanyanyasa wa toto na kuwafanyia vitendo vya ukatili hali inayopelekea watoto kukosa haki zao za msingi kama vile elimu na kuharibu ndoto zao kitu ambacho ni kosa na kinyume cha sheria.
Aidha galawa ameongeza watoto wengi wanafanyiwa vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na kuwa achisha shule na kuwaozesha na wengine wanawapeleka watoto wao mjini wakfanye kazi za ndani kitu ambacho ni kosa na mzazi yeyote atakaye kamatwa anafanya vitendo hivyo atachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na kwenda jela miaka 30.
Mmoja wa watoto hao valeliusi mwakasanga amesema kuwa wazazi wengi wilayani momba hawatoi ushilikiano kwa walimu na hawana mwamko juu ya elimu kwani wengi wao hawawapatii watoto wao mahitaji mhimu ya shule kama vile sale za shule na vifaa vya kujifunzia wakidai ni masikini huku kila siku wanahuzulia vilabuni kunywa pombe na wanatoa fedha .
Kwa upande wake kaimu afisa ustawi wa jamii mkoa wa songwe gift schone amesema kuwa wamejipanga kukabiliana na vitendo hivyo huku vikipungua kwa kiasi kikubwa kutoka 90% hadi 40% kwa mkoa wa songwe hii ni kutokana na jitihada za idala ya afya kupitia kitengo cha ustawi wa jamii .



Post a Comment