Header Ads


MTU MMOJA MKAZI WA ITAMBULA WILAYANI MOMBA MKOANI SONGWE AMEGONGWA NA GARI NA KUFARIKI PAPO HAPO.

Mbozi-Songwe
Na zefrine machesha
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la ernest Gabriel (25) mkazi itumbula kamsamba wilayani momba mkoani songwe amefaliki dunia baada ya kugogwa na gari lenye namba za usajili T303 CRW noah katika eneo la mwaka tunduma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani songwe matius lukasi nyange amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana juni 13 mwaka huu saa sita mchana  katika barabara ya tunduma - sumbawanga .
Kamanda nyange ameongeza kuwa  gari lenye namba T 303 CRW aina ya noah ikiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika na alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea ilimgonga mtembea kwa miguu na kumsababishia kifo chake papo hapo
Aidha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi alikuwa nao dereva huyo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitari ya tunduma na jitihada za kumsaka dereva huyo zinaendelea.
Kamanda nyange ametoa wito kwa watumia barabara na wananchi wawe waangalifu wawapo barabarani pia madereva kutumia spidi zinzoruhusiwa hasa wanapofika karibu na makazi ya watu ili kupunguza vifo vinavyo weza kuepukika .

No comments

Powered by Blogger.