LICHA YA KUWEPO KWA MRADI WA MAJI KATIKA KATA YA HALUNGU ULIOGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILIONI 600 LAKINI BADO WANANCHI WA KATA HIYO WANAKABILIWA NA UHABA MKUBWA WA MAJI
Mbozi-Songwe
Na. zefrine machesha
Wakizungumza wakati wa ziara ya kamati ya fedha,mipango,uchumi na uongozi katika kata ya Halungu wananchi wa kata hiyo wamesema kuwa mradi huo umejengwa 2010 ukiwa na kina cha mita 10 lakini bado maji si ya kutosha katika maeneo yao kwa baadhi ya vituo kutokutoa maji.
Katibu wa mradi huo Edison Mwangobola amesema tenki la mradi huo lipo chini ya kiwango na wakati mwingine huvuja huku mabomba yakikosa air valvu ambapo wanalamika kutoboa kwa misumari ili hewa ipenyena kuitaka serikali izijengee geti valvu eneo maalum kuliko kuzifukia ardhini.
Naye Mathias Simkoko mkazi wa kata hiyo amesema kuwa mkuu wa wilaya aliahidi mwezi april kuwa majio yataanza kutoka ndani ya siku saba lakini mpaka sasa yako kimya maji hayo hayatoki na wananchikuendelea kupata adha ya maji kwa kuendelea kutumia maji ya visima vifupi ambayo ni machache.
Akizungumzia suala hilo mhandisi wa idara ya maji wilayani Mbozi Cyprian Warioba amesema kilichochelewesha ni mfumo wa manunuzi wa serikali ambao una mlolongo mrefu na kuahidi kuwa tayari wamekamilisha hilo na watakamilisha mradi huo wiki ijayo wakati huohuo mwenyekiti wa halimashauri Erick Minga akiwatakja jumatatu wafike katika mradi huo ili maji yaanze mara moja kutoka ili kuwapunguzia adha wananchi hao.

Post a Comment