Header Ads


MAKAMU WA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASANI AMEWAAGIZA WAKUU WA WILAYA NCHINI KUCHUKUA HATUA SITAHIKI KATIKA KULINDA NA KUHIFADHI MAZINGIRA.

Mbeya
Na.zefrine machesha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuchukua hatua stahiki katika kulinda na kuhifadhi mazingira katika wilaya zao ili kukabiliana uharibifu mkubwa wa mazingira kwenye misitu na vyanzo vya maji ili visikauke na kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Kikosi Kazi cha Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa mkoa wa huo Amos Makalla kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji katika wilaya za Mbarari na Chunya .
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la uharibifu wa mazingira katika baadhi ya wilaya nchini ni kubwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Wakuu wa wilaya kwa ushirikiano na watendaji wengine katika kukabiliana na hali hiyo kwenye maeneo yao.
Makamu wa Rais pia amepongeza timu ya wataalamu wa kikosi kazi cha Mkoa wa Mbeya kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya inayolenga kuokoa mfumo wa ikolojia katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amemweleza Makamu wa Rais kuwa aliamua kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa mpaka kati ya wananchi wa wilaya ya Chunya na Mbarali na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, uharibifu wa mazingira na upotevu wa maji kwenye Mto Ruaha Mkuu.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla baada ya kukabidhi taarifa ya kikosi kazi kwa Makamu wa Rais amesema kikosi kazi hicho kimependekeza vijiji Tisa kati ya 33 ambavyo vina mgogoro na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha viondolewe kabisa kwenye eneo la hifadhi na vijiji vingine Vinne vinatakiwa kufutwa na wananchi kuhamishwa kwenye maeneo hayo na Serikali itawalipa fidia na kuratibu eneo watakapohamishiwa.

No comments

Powered by Blogger.