MKUU WA WILAYA YA IRINGA RICHARD KASESELA ALAZIMIKA KUOKOA MAITI YA MCHIMBAJI WA MADINI
Iringa
Na.zefrine machesha
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amelazimika kufanya kazi ya uokoaji wa maiti ya mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala bwana Vaspa nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa takribani masaa kumi na nane
Kasesela amesema kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa mbili asubuhi jana alipowasili katika mgodi huo wa Nyakavangala lakini yeye,waandishi wa habari na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa walijitahidi kuokoa mwili wa marehemu hadi majira ya saa saba na dakika 50 usiku ambapo mwili huo ulipatikana.
Kwa upande wake Chief inspector Mayunga Ngele amewataka wachimbaji wote kutochimba tena kwenye mashimo yaliyozuiliwa ili kuepusha ajali mbalimbali hapo mgodini kwa kuwa hata huyo marehemu na wenzake walikatazwa kuchimba katika shimo hilo ambalo lilikuwa kwenye hali mbaya ya kuanguka.
Mmiliki wa mgodi wa Nyakavangala Thomas masuka amemshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa jitihada zake za kuhakikisha kila kitu kinanda kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali na kuahidi kuwa gharama za kuuokoa mwili hadi kuufikisha kwa ndugu atagharamia.

Post a Comment