Header Ads


JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

MBEYA.
 Na zefrine machesha

Jeshila polisi mkoani mbeya linawashikilia watu wawili ally joseph [67] na daud ally [32] wote wakazi wa kijiji cha ipinda wilayani mbeya kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi ambalo ni kosa na kinyume na sheria.
Akithibitisah bkutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa mbeya naibu kamishina wa polisi dhahiri   kidavashari amesema kuwa  mnamo tarehe 13.06.  Kuanzia majira saa 17:00 jioni hadi saa 19:00 usiku, jeshi la polisi mkoa wa mbeya lilifanya msako katika  kijiji cha ipinda kilichopo kata ya ihango, tarafa ya iyunga, wilaya ya mbeya vijijini, mkoa wa mbeya.
Katika msako huo, watu wawili walikamatwa wakiwa na bhangi, ambapo ally joseph [67] mkazi wa kijiji cha ipinda ambaye alikamatwa akiwa na bhangi kavu debe 01 iliyokuwa imehifadhiwa kwenye mfuko wa salfeti na  mtuhumiwa daud ally [32] mkazi wa kijiji cha ipinda ambaye alikamatwa akiwa na bhangi kilo 05 na miche 670 ya bhangi ambayo alikuwa ameipanda kwenye shamba la mahindi.
Imeelezwa kuwa watuhumiwa ni wauzaji na wakulima wa bhangi na  watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Aidha kidavashari ametoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji na   kuwataka  wananchi kuendelea kutoa taarifa za mtu/watu au kikundi cha watu wanaojihusisha na kulima, kuuza/kusambaza dawa za kulevya [bhangi] ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

No comments

Powered by Blogger.