WANANCHI WILAYNI KYELA MKONI MBEYA WALALMIKIA MRADI WA MAJI KUTELEKEZWA ZAIDI YA MIAKA MINNE SASA
MBEYA
WANANCHI
wa vijiji vilivyopo kata za Ipinda ,Ipande,Mwaya,Muungano Talatala na
Ikama ,wameilalamikia halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuutelekeza mradi
wa maji safi na salama wa zaidi ya Bilioni 3.8 huku wakazi wa maeneo
hayo wakiendelea kuhatarisha maisha yao kwa kunywa maji machafu.
Wakizungumza
jana na gazeti hili baada ya kufanya ziara ya siku moja kuutembelea
mradi huo kwa masaa saba,walisema tatizo la maji safi na salama Kyela ni
sugu,hivyo serikali ilitoa Bilioni 3.8 kwa ajili ya kujenga mradi wa
maji safi ili wakazi wa kata hizo waweze kunufaika lakini umetelekezwa
na hakuna mrejesho.
Asha
Kimbe mkazi wa Talatala,alisema ni ajabu kuona halmashauri imeshindwa
kufuatilia waliosababisha kuukwamisha mradi huo kutokana na umuhimu wake
na kwamba wanaiomba serikali kuu kuingilia kati ili kuhakikisha mradi
unamalizika na kuwawajibisha walioukwamisha.
Sanke
Mwaitamwa mkazi wa Ipinda alisema mradi huo ulikuwa ni muhimu sana
ambapo ulianza kutelekezwa miaka minne iliyopita ambapo wao kama
wananchi wameshindwa kuelewa kinachoendelea licha ya kuwa waliwauliza
madiwani wao pasipo kuwapa majibu ya kutosha.
Alisema
kukosekana kwa mradi huo wa maji bado maisha yao yapo hatarini kwa
kuendelea kunywa maji ya mtoni ambayo hata hivyo si safi na salama hivyo
kupelekea kuuguma magonjwa ya milipuko kikiwemo kipindupindi ambacho
kimekuwa kikiibuka kila mwaka na kuua watu.
Akizungumza
kwaniaba ya madiwani wenzake,diwani wa kata ya Talatala,Angumbwike
Mwakibete alisema ni kweli mradi huo umetelekezwa tangu miaka minne
iliyopita na kwamba waliwahi kukaa vikao na madiwani ambao vijiji vyao
vingenufaika na mradi huo,na kusema kuwa suala hilo lilipelekwa ngazi ya
wilaya ambako linashughulikiwa.
Akijibu
utelekezwaji wa mradi huo,Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
hiyo,Dkt,Hunter Mwakifuna,alisema ni kweli fedha za ujenzi wa mradi huo
wa maji safi na salama zilitoka zaidi ya Bilioni 3.8 lakini mradi
uletelekezwa miaka minne iliyopita na kusema kuwa wakati huo yeye hakuwa
mwenyekiti.
Alisema
mradi huo ukikamilika utasaidia vijiji vya Kiingili kata ya
Ipinda,Bukinga na Lutusyo kata ya Muungano,Kagogo na Ngolele kata ya
Talatala,Mwambusye kata ya Ikama na Ndola,Lughombo kata ya Mwaya,na kuwa
kukwama kwa mradi huo kumeongeza hadha ya upatikanaji wa maji kwa
wakazi wa kata hizo.
Alisema
mradi huo ulitolewa mwaka 2014 ambapo hadi sasa ni miaka minne imepita
tangu mradi utelekezwe na kwamba kwa kuwa yeye ni mwenyekiti na ni
diwani kata ya Ipinda ameanza mchakato wa kulipeleka suala hilo ngazi ya
mkoa ili kuhakikisha linafanyiwa kazi.
Post a Comment