Header Ads


ZAIDI YA NYUMBA 30 ZAEZULIWA NA NYINGINE KUBOMOKA KATA YA NAMING'ONGO WILAYA YA MOMBA KUFUATIA MVUA KUBWA KUNYESHA







Momba
Zaidi ya nyumba 30 katika kitongoji cha nachinsitu kata ya naming’ongo wilayani momba mkoani songwe zimeezuliwa huku nyingine zikibomoka kufuatia mvua kubwa zilizokua zimeambatana na upepo kunyesha katika kata hiyo.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 10 jion ambapo mvua kubwa zilizokua zimeambatana na upepo zilinyesha kwa muda wa saa moja na kusababisha madhara hayo makubwa.
Jitihada za kumtafafuta mwenyekiti wa kitongoji cha nanchisitu kuzungumzia tukio hilo zimegonjwa mwamba baada ya kutokupatika wakati wote.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha kawana ambaye pia ni kaimu mtendaji wa kijiji cha namingo’ngo kilian sikananga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema licha ya kuezea nyumba 34 na nyingine kubomoka katika kitongoji hicho mvua hizo pia zimeezua madarasa mawili ya shule moja ya msingi kijijini hapo na ofisi moja ya walimu.
Kaimu mtendaji kijiji hicho ameongeza  mvua hizo pia zilisababisha  mafuriko katika kitongoji cha kawana hali iliyowafanya baadhi ya wananchi kukosa mahali pa kukaa mpaka maji hayo yalipo kauka siku ya pili yake jana .

No comments

Powered by Blogger.