MKUU WA MKOA WA RUKWA AMEWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS JOHN MAGUFULI ILI AWEZE KUWAONGOZA WANANCHI KWA HAKI
RUKWA
MKUU
wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaomba viongozi wa dini mkoani humo
kuendelea kumuombea rais John Magufuli pamoja na watendaji wengine wa
serikali ili aweze kuwaongoza wananchi kwa kuzingatia misingi ya haki usawa na
kuwaletea maendeleo endelevu.
aliyasema hayo wakati akichangia
shilingi milioni moja kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo
la kusaidia ujenzi wa kituo cha afya cha Waislamu kinachoendelea kujengwa
katika Tarafa ya Kirando, Kata ya Kirando Wilayani Nkasi mkoani humo.
Alisema kuwa rais na watendaji wa
serikali ya awamu ya tano wanaitaji kuombewa daima kwani kufanya kazi ya
kuwaongoza wananchi sio lelemama hivyo unahitajika msaada wa Mwenyezi Mungu.
Wangabo alisema katika kuwaongoza
watu wapo waadilifu na wenye nia njema kwa taifa lakini pia wapo watu ambao ni
wasaliti na hawanania njema kwani wanatanguliza masuala binafsi ikiwemo
ubadhirifu, rushwa na matendo mengine ambayo si mazuri kwa mwenyezi Mungu na
wananchi pia
mkuu huyo wa mkoa
alisema kuwa taasisi za kidini kwa
muda mrefu zimekuwa zikisaidia juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma
muhimu zinawafikia wananchi jambo ambalo pia linasaidia utekelezaji wa Ilani ya
chama tawala inayoongoza serikali.
Aidha alitoa mchango huo kwa lengo
la kuzindua harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya katika
siku ya maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Kimkoa
katika Kijiji cha Kabwe, Kata ya Kabwe wilayani Nkasi ambapo alikuwa rasmi
katika sherehe hizo.
Hata hivyo aliwashukuru waumini wa
madhehebu mbalimbali kwa kuendelea kuiombea serikali na kusisitiza
kuendelea kuhubiri amani iliyopo ili nchi isonge mbele katika sekta zote na
wananchi waweze kufurahia amani, utulivu na uhuru wa kuabudu.
Kwaupande wake katibu wa Bakwata
mkoa wa Rukwa Mohammed Khatibu alipokuwa akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
alisema kuwa Baraza hilo linahitaji kiasi cha shilingi 6,910,000 ili kuweza
kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya ambacho kipo katika hatua ya upauaji.
Post a Comment