WATENDAJI WAWILI WATUMBULIWA AKIWEMO AFISA UGAVI KWA ULEVI NA WIZI
ILEJE-SONGWE
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya ileje Haji Mnasi,alisema afisa ugavi baada ya
kuendekeza ulevi,walimuonya ambapo alidai hatorudia lakini haiklupita wiki moja
tangu aombe radhi akajabainika kuwa na kinywaji cha pombe kali ofisini.
Alisema
baada ya kukutwa na pombe kali ofisini ndipo madiwani wakaona ni bora mtu huyo
atimuliwe ili nafasi yake ichukuliwe na mtu atakayekuwa tayari kufanya kazi kwa
kufuata sheria na tayari nafasi yake imezibwa.
Mbunge
jimbo la Ileje Janneth Mbene akaeleza kusikitishwa na kitenda hicho na kudai
kuwa kitendo kilichofanywa na madiwani hao kinapaswa kupongeza kwa kuwa
watendaji wengi wanaifanya Ileje kuwa shanba la bibi.
Mkuu
wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude alisema hatua hiyo iliyofanyika italeta heshima
kwa watendaji wasio waaminifu na kwamba serikali ya sasa haipotayari kuwalinda
watendaji wazembe.
Wafanyakazi
waliokuwa katika hatari ya kuondolewa kazini ni wanne, baada ya uongozi wa
wilaya na baraza kujiridhisha wameazimia kuwafukuza kazi watendaji 2, mmoja
ambaye ni Emmanuel mwenisongole aliyekuwa akichakachua stakabadhi za
halmashauri na kujipatia fedha bado shauri lake linachunguzwa, wakati mwingine
katika idara ya afya Anna Mwakipesile amerejea kazini baada ya kukutwa
hana hatia.
Post a Comment