SIMBA YAAMBULIA SARE AFRIKA KUSINI, MECHI YACHEZWA ASUBUHI
Timu ya Simba ambayo ipo nchini Afrika Kusini ilipoweka kambi kujiandaa kwa msimu mpya, imeshuka uwanjani leo na kupata matokeo ya sare ya -1 dhidi ya Bidvest Wits.
Timu hizo zilikutana kwenye Uwanja wa Sturrock Park, Chuo Kikuu cha Afrika Kusini asubuhi ya leo ukiwa ni mchezo wa kirafiki.
Erasto Nyoni ambaye amesajiliwa hivi karibuni, ndiye aliyeanza kuifungia Simba katika dakika ya 33 kabla ya wenyeji kusawazisha baadaye.
Baada ya mchezo huo, Simba inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kwa ajili ya mchezo mwingine wa kujipima nguvu dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Agosti 8, mwaka huu katika Tamasha la Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Post a Comment