WANANCHI WA KIJIJI CHA LUKULULU NA KIJIJIJI CHA MBEWE KATA YA MLANGALI WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE WAMETAKIWA KUKATA BIMA YA AFYA
MBOZI -SONGWE
Hayo
yamesemwa na mbunge wa jimbo la vwawa japhet hasunga alipokuwa kwenye ziara
yake ya kusikiliza kelo za wananchi wa vijiji hivyo ambapo amesema kuwa
wananchi hao wanatakiwa kujiunga na mfuko wa bima kwa manufaa yao wenyewe .
Baadhi ya
wananchi rehema mwashitete na wilisoni wenela wakati wakitoa kero zao wamesema
kuwa kero yao ni miundombinu mibovu ,pembejeo feki, ambapo wamekuwa wakiuziwa
mbegu feki na kuludisha nyuma maendeleo ya kilmo wilayani mbozi.
Kwa upande
wake afisa kilimo kata ya teofil mwakalile amesema kuwa serikali imejipanga
kukabiliana na changamoto hiyo ambapo amewahakikishia wananchi kununua pembejeo
kwa mawakala wanaofahamika na kuhakikisha wa nachukua risti ili iwe rahisi
kumkamata endapo atauza pembejeo feki.
Kwa upande
wake diwani wa kata ya mlangali na mwenyekiti wa halimashauri ya mbozi Eliki
ambakisye amewtaka wananchi kutunza misitu na vyanzo vya maji ikiwa na pamoja
na kuacha kufanya shughuri za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji kwa faida ya
sasa na kizazi kijacho.
Post a Comment