DC ILEJE ABAINI UFISADI WA MILIONI 62 MALIPO YA MNARA WA SIMU ZILIZOKUWA ZIKILIPWA KWENYE AKAUNTI HEWA.
Ileje-Songwe
SERIKALI wilayani Ileje mkoani Songwe imebaini ufisadi wa zaidi ya shilingi million 60 fedha za upangishaji wa mnara wa vodacom ambazo zimekuwa zikiingizwa kwenye account hewa iliyotajwa kumilikiwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Regina Nginila ambaye taarifa za makazi yake hazijulikani huku akidaiwa kujitwalia eneo la serikali kinyemela na kuingia mkataba na kampuni hiyo ya simu.
Akizungumza jana mbele ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe, mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkude, ametaja ufisadi unaofanyika kwenye mradi wa upangishaji minara katika milima ya itumba, na kumtaja mmiriki wa ardhi hiyo kwa jina la Regina Nginila, ambalo hata lillipochunguzwa limebainika kuwa ni jina hewa.
''Kitendo kilichofanyika kimeni kera sana na ndiyo maana aliyekuwa afisa ardhi wa hapa aliyehamia Bagamoyo nilimuita baada ya kukuta sahihi yake kwenye ofa ya kiwanja mali ya serikali na sasa jina lake tumelihifadhi kwa kuwa yupo kwenye uchunguzi''alisema Mkude.
Haji Mnasi ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, alisema kuwa mkataba huo ni hewa, na umeikosesha mapato Serikali ya shillingi million 62 ,na kwamba kwa sasa wataanza ukaguzi wa mikataba yote iliyopo kwenye halmashauri, ili wilaya ya Ileje isiwe tena shamba la bibi.
Mohammed Maliyao diwani kata Itumba wa halmashauri hiyo,ambao wameeleza wazi kutilia shaka juu ya uharali wa vibali vya umiriki wa eneo la upangishaji wa mnara huo, ambapo wameunga mkoano jitihada za viongozi wa Serikali za kubaini wizi huo.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya hiyo, ni kuwa afisa ardhi aliyeidhinisha makubaliano hayo, anashikiliwa hadi hivi sasa kwa mahojiano,na kwamba tayari wameanza kutajana, huku mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Galawa, akieleza mpango wa kuunda timu ya mkoa.
Galawa alisema Timu atakayoiunda itachunguza mikataba yote ya upangishaji wa minara, lengo ni kunusuru halmashauri,zikiwemo mpya kuingia kwenye mitego ya aina hiy na ufisadi unayoikosesha mapato serikali.
Post a Comment