WANANCHI WA KITONGOJI CHA KALASHA KATA YA MLOWO WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDIII BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA
MBOZI -SONGWE
Hayo
yamesemwa na mfanyabiashara wiliam mgogo katika hafra ya kuukaribisha uongozi
mpya wa chama cha mapinduzi kitongoji cha kalasha ambapo amesema maendeleo
yanaletwa kwa jitihada za wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao ambapo
amewataka viongozi waliochaguliwa kutumia hekima na busala katika kutoa
maamuzi.
Mgogo
amemshukuru abonike kibona mwkt mstaafu kwa kazi nzuri aliyoifanya kipindi cha
uongozi wake ambapo amemtaka fastoni nzowa kufata nyayo hizo na kuendeleza
maendeleo ya kalasha na kata ya mlowo.
John paza
katibu wa ccm tawi la kalasha amesema
kuwa kiongozi aliyemaliza mda wake alikuwa kiongozi bora hivyo wakaamua kufanya
hafra hiyo ya kumuaga ili kuonyesha upendo kwa viongozi hao.
Post a Comment