Header Ads


MBUNGE WA VITI MAARUMU MKOA WA SONGWE (CHADEMA) RISALA KABONGO AMETOA MACHOZI MBELE YA UMATI WA WATU





MBOZI-SONGWE
Kabongo ametoa machozi wakati alipotembelea kituo hicho ikiwa ni ziara yake ambayo ameifanya mwishoni mwa wiki ikiwa ni kusherekea miaka 25 ya chadema kwakutembelea  vituo vya afya na hospitari ya wilaya vywawa , hospitali ya mbozi misheni ambapo ametoa mashuka zaidi ya 350 ili kupunguza changamoto ya uhaba wa mashuka.

Kabongo pia ametoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima katika kituyo cha mbozi misheni kama unga ,kalanga, sabuni za unga sabuni za mche , sukari, chumvi ,biskuti, pipi,pamoja na mashuka 20 ambapo ametoa pongezi kwa uongozi wa kituo hicho kwa malezi mazuri wanayoyatoa kwa watoto hao na kuahidi kuendelea kutoa ushilikiano.

Mganga mkuu wa hospitari ya wilaya vwawa  janeth makoye ameshukuru kwa msaada wa mashuka 100 na kuomba wadau wengine waige mfano ili kusaidia  kupunguza changamoto katika hospitari hiyo.

Kwaupande wake katibu wa kituo  cha kulelea watoto yatima joseph olomy  ameshukuru kupata misaada hiyo na kuomba wadau mbalimbali waguswe kuwasaidia watoto hao kwa namna mbalimbali.

No comments

Powered by Blogger.