TETESI ZA USAJIRI LEO TAREHE 3.8.2017
MACHESHAZEFRINE.BLOGSPOT.COM inakuletea muhtasari wa tetesi na habari za uhamisho kutoka Ligi Kuu Uingereza, La Liga, Serie A, Bundesliga na kwingineko
MBAPPE AWAAMBIA MONACO ANATAKA KUONDOKA
Kinda wa Monaco, Kylian Mbappe ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka kipindi hiki cha uhamisho majira ya joto, kwa mujibu wa L'Equipe .
NEYMAR KUIGHARIMU PSG £450M
Neymar aitaigharimu Paris Saint-Germain kitita cha paundi milioni 450 kukamilisha usajili wake kutua Paris akitokea Barcelona, kwa mujibu wa Sky Sports .
VAN DIJK ANAJARIBU KUSHINIKIZA KUTUA LIVERPOOL
Virgil van Dijk ameonesha ishara kuwa hataki kuendelea kubaki Southampton na anataka kushinikiza kujiunga na Liverpool, kwa mujibu wa the Mirror .
NAMBA YA NEYMAR PSG YAFAHAMIKA
Neymar atavaa jezi nambari 10 katika kikosi cha Paris Saint-Germain mara uhamisho wake kutoka Barcelona utakapokamilika, kwa mujibu wa Mirror .
BARCA KUTOA €120M KWA AJILI YA COUTINHO
Barcelona wanapuuzia madai ya Liverpool kuwa Philippe Coutinho hauzwi kwa bei yoyote na wameshatenga euro milioni 120 kwa ajili ya Mbrazili huyo, kwa mujibu wa the Daily Mail .
EVERTON YAPIGANA VIKUMBO NA LIVERPOOL KUMWANIA MOR
Everton wameungana na Liverpool, Roma, Fiorentina, na Inter katika mbio za kumfukuzia kinda wa Borussia Dortmund Emre Mor, kwa mujibu wa The Sun .
ARSENAL WANATARAJIA ALEXIS ATAONDOKA
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez amewaambia wachezaji wenzake wa Emirates kuwa anatarajia kuondoka klabuni hapo msimu huu, kwa mujibu wa Daily Mail .
ARSENAL YAPIMA DAU LA SERI
Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumsajli kiungo wa mahiri wa Nice Jean Michael Seri, kwa mujibu wa ESPN .
Habari zinadai kuwa Washika Mtutu hao wamejipanga kuchuana na Tottenham kuipata saini ya Seri.
DI MARIA YU TAYARI KUTUA BARCA
Neymar akiwa mbioni kujiunga na Paris Saint-Germain, Barcelona wamekuwa karibu na Angel Di Maria wakitaka kumsajili Mwargentina huyo kama mbadala wake, Mundo Deportivo limeripoti.
AC MILAN WANAMTAKA DIEGO COSTA
AC Milan wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa kwa mkataba wa kudumu katika dirisha la uhamisho wa majira ya joto, kwa mujibu wa habari kutoka Telegraph .
Kocha wa Blues Antonio Conte ameweka bayana kuwa Costa hayumo kwenye mipango yake katika michuano ya Ligi Kuu Uingereza msimu ujao.
MBAPPE BEI YAKE SASA NI €200M
Monaco imepandisha bei ya Kylian Mbappe hadi euro milioni 200 wakiamini kuwa Barcelona watahitaji kumsajili Mfaransa huyo kuziba pengo la Neymar anayekaribia kutua PSG Mail Online .
Real Madrid kwa mujibu wa habari wapo tayari kutoa paundi milioni 160 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, lakini sasa watalazimika kujikaza kupata fedha zaidi kufanikisha usajili huo.
CHELSEA WANANAMTAKA DRINKWATER
Chelsea wamemuongeza Danny Drinkwater wa Leicester kwenye orodha ya wachezaji wanaotaka kuwasajili majira ya joto, kwa mujibu wa Telegraph .
Antonio Conte bado anataka kukipanga vema kikosi chake baada ya kumpoteza Nemanja Matic aliyejiunga na Manchester United.
CHELSEA YAMRUDIA CANDREVA
Chelsea wanaamini watafanikiwa kumsajili Antonio Candreva wa Inter, miamba hao wa Serie A pia wanataka kumsajili nyota wa Lazio Keita Balde, kwa mujibu wa Mirror .
LIVERPOOL YAJIUNGA KATIKA MBIO ZA SANCHES
Liverpool wameungana na Chelsea na Manchester United katika mbio za kumuwinda kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, kwa mujibu wa Sport Bild .
KLABU TANO ZINAMTAKA SMALLING
Klabu tano za Ligi Kuu Uingereza zinaitaka saini ya beki wa Manchester United Chris Smallaing, kwa mujibu wa TMW .
West Brom wamekuwa wakiihitaji saini ya Muingereza huyo na sasa imefuatiwa na Burnley, Leicester, Crystal Palace na Stoke.
GRIEZMANN APEWA SHAVU KUMRITHI NEYMAR
Barcelona watafanya jitihada kumsajili nyota wa Atletico Madrid Antoine Griezmann kuziba pengo la Neymar mwenye dalili zote za kujiunga na PSG, kwa mujibu wa SPORT .
Habari zinadai kuwa Blaugrana watakuwa tayari kumwachilia Neymar kuondoka na wametoa orodha ya wachezaji wanaoamini wataweza kuziba nafasi yake, miongoni mwao ni, Borussia Dortmund's Ousmane Dembele na PSG's Angel Di Maria.
NEYMAR NEYMAR KUFANYIWA VIPIMO PSG
Mshambuliaji wa Barcelona atafanyiwa vipimo Doha Jumanne kukamilisha uhamisho wake wa euro milioni 222 kujiunga na miamba wa Paris, PSG kwa mujibu wa Al Watan .
Mchezaji huyo amehusishwa na tetesi za kutua kwenye klabu hiyo ya Ligue 1 ambao wanaweza kukamilisha uhamisho wake kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
MAN UTD YAKUBALI MASHARTI YA AURIER
Manchester United wamefikia makubaliano ya kukamilisha dili la kumsajili Serge Aurier kumsajli beki huyo wa kulia kutoka PSG lakini watalazimika kuikabili mahakama kumruhusu mchezaji huyo kiingia Uingereza kwa mujibu wa The Mirror .
LIVERPOOL WANAMTAKA LEMAR
Liverpool wanaweza kuingia kwenye mbio za kumsajili Thomas Lemar kutoka Monaco ikiwa Philippe Coutinho atajiunga na Barcelona, kwa mujibu wa Le10 Sport .
BARCA INAWEZA KUMGEUKIA OZIL NEYMAR AKIONDOKA
Barcelona inaweza kugeuzia rada kwa Mesut Ozil wa Arsenal ikiwa watashindwa kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool, Don Balon kimedai.
Mustakabali wa Neymar bado ni sintofahamu kwani muda wowote anaweza kukamilisha uhamisho wake kutua PSG.
Post a Comment