Header Ads


JESHI LA POLISI MKOANI SONGWE LINAMSHIKILIA MBUNGE WA JIMBO MBOZI PASCAL HAONGA



MBOZI-SONGWE
Jeshi la polisi mkoani songwe linamshikilia mbunge wa jimbo mbozi pascal haonga kwa tuhuma za kutoa lugha ya uchochezi kwa kuwahamasisha wananchi na madereva kwenda katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa SONGWE Chiku Galawa kumtaka kutengua uamuzi wa kusitisha usafiri wa Malori.

Akithibitisha kukamatwa kwa Mbunge wa Jimbo hilo kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Mathias Nyange amesema kuwa ni kweli wananmshikilia mbunge huyo kwa kutoa lugha ya kichochezi kwa kulazimisha watu wavunje sheria kupanda malori na kuwa  wakimaliza upelelezi  watamfikisha mahakamani.

Aidha nyange amesema sheria zimetungwa zipo nz watu wanatakiwa kuzifuta sheria hizo na  wananchi waache kufuata maneno ya kichochezi ya watu wanaotaka kuvunja sheria ambazo wamezitunga wao wenyewe.
 
mbunge wa jimbo la mbozi pascal haonga

Akizungumzia kukamatwa kwa mbunge huyo mwanasheria wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Boniface Mwabukusi amesema kuwa wameshindwa kupata dhamana ya mbunge huyo kwa kuwa kesi ya mbunge huyo iko chini ya ofisa upelelzi wa polisi mkoa wa Songwe ambaye hakuwepo wakati huo hivyo wanatarajia kufika leo katika makao makuu ya jeshi hilo ili kujua kama watapewa dhamana ama hapana.
  
Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA James Mbasha akizungumza nje ya makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Songwe amesema kuwa suala hilo limekaa kiuonevu kufuatia baadhi ya maeneo katika jimbo la vwawa wananchi kuendelea na kutumia usafiri huo hivyo serikali ijali majukumu ya mbunge ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki ikiwemo usafiri.

No comments

Powered by Blogger.