TETESI ZA USAJILI LEO IJUMAA 11.8.2017
Macheshazefrine.blogspot inakuletea muhtasari wa tetesi na habari za uhamisho kutoka Ligi Kuu Uingereza, La Liga, Serie A, Bundesliga na kwingineko
MOU YAPAMBANA KUMSAJILI BALE KWA £100M
Jose Mourinho ameitaka Manchester United kutoa dau la paundi milioni 100 kwa ajili ya nyota wa Real Madrid Gareth Bale, kwa mujibu wa habari kutoka The Sun .
Licha ya mchezaji huyo wa zamani wa Spurs kufunguka hadharani kuwa hana mpango wa kuondoka Real Madrid, Mreno Mourinho anaamini bado inawezekana kumshawishi kuondoka Bernabeu kwa ujira wa paundi 500,000 kwa wiki.
CHELSEA KUMSAJILI BARKLEY
Chelsea inazidi kuwa tishio kwa Tottenham katika mbio za kumwania Ross Barkley kwa mujibu wa The Daily Telegraph .
SPURS KUTOA DAU LA £35M KWA AJILI YA BEKI WA AJAX
Tottenham wapo tayari kutoa dau la paundi milioni 35 kwa ajili ya beki wa Ajax Davinson Sanchez, kwa mujibu wa The Sun .
Mauricio Pochettino bado hajafanya manunuzi yoyote msimu huu wa majira ya joto, lakini mdachi huyo amekuwa shabaha yake kuu, ingawa Chelsea, Barcelona na Crystal Palace zinataka kumsajili mchezaji huyo pia.
WEST HAM YAMWANDALIA OFA CARVALHO
West Ham United wapo tayari kutoa ofa ya paundi milioni 25 kwa ajili ya mchezaji wa Sporting Lisbon, William Carvalho, limeripoti gazeti la Daily Mail .
Mchezaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 amekuwa kwenye rada za klabu kadhaa za Uingereza, na Sporting inataka kumuuza kwa kiasi kisichopungua paundi milioni 39.5.
CHELSEA TAYARI KUTOA £35M KWA AJLI YA OX
Chelsea wapo tayari kuijaribu Arsenal kumwachilia Alex Oxlade-Chamberlain kwa dau la paundi milioni 35, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amebakiwa na mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake na Gunners, na Antonio Conte atatoa dau nono kumshawishi Wenger kukubali kumuuza.
ZLATAN ATAMANI KUREJA MAN UNITED
Zlatan Ibrahimovic amemwambia Jose Mourinho kuwa anataka kujiunga tena na kikosi cha Manchester United mara atakapopona majeraha yake, kwa mujibu wa Daily Mail.
BARCA YATAKIWA KULIPA £135M KUMPATA DEMBELE
Barcelona imeambiwa italazimika kulipa paundi milioni 135 kwa ajili ya Ousmane Dembele kwani Borussia Dortmund bado wanatamani kubaki na mchezaji wao muhimu, kwa mujibu wa Guardian .
Barca wanaamini Dembele atakuwa mbadala sahihi wa Neymar ambaye ametimkia PSG kwa dau la rekodi ya dunia la paundi milioni 198 uhamisho wa majira ya joto.
MBAPPE ACHAGUA KUTUA PSG
Kylian Mbappe ameamua anataka kujiunga na PSG miamba hao wa Ligue 1 wanapojipanga kutoa ofa ya euro milioni 155 kwa ajili ya nyota huyo wa Monaco, Telefoot limeripoti.
PSG KUTOA £80M KWA AJILI YA ALEXIS
Jitihada za Arsenal kumbakisha Alexis Sanchez zinaweza kuharibiwa na dau la paundi milioni 80 ambazo PSG inaandaa kwa ajili ya mchezaji huyo wa Chile, kwa mujibu wa The Sun .
BARCELONA YAKUBALI DILI KUMSAJLI COUTINHO
Barcelona imefikia makubaliano na klabu ya Liverpool kumsajili nyota matata wa Kibrazili Philippe Coutinho kwa mujibu wa ESPN Deportes .
MAN UTD & INTER ZAMWANIA ROSE
Manchester United na Inter zimepata fununu kuwa Danny Rose wa Tottenham anatarajia kurejea mzigoni baada ya majeraha ya muda mrefu, kwa mujibu wa Mirror .
Klabu hizo mbili zinataka kujiimarisha zaidi kwa ajili ya msimu mpya na Mashetani Wekdundu na Nerazzurri wameshatenga madau ya maana.
LIVERPOOL KUMRUDIA VAN DIJK
Liverpool itatoa dau la paundi milioni 60 kwa ajili ya Virgil van Dijk baada ya neki huyo wa kati kuomba kuihama Southampton kwa mujibu wa Express .
Chelsea pia ni klabu nyingine inayotaka kumsajli mchezaji huyo, lakini inaaminika kuwa Antonio Conte anatamani zaidi kusajili beki wa pembeni, Serge Aurier wa PSG ndiye mchezaji anayemtaka.
MOURINHO AMGEUKIA FABINHO USAJILI WA MAJIRA YA JOTO
Chanzo cha Hispania Don Balon kimedai kuwa Jose Mourinho amekasirishwa na matatizo ya beki wa PSG Serge Aurier kukosa viza ya kuingia Uingereza.
Kwa maana hiyo basi, bosi huyo wa Manchester United amemgeukia mchezaji machachari wa Monaco Fabinho, na inaaminika ametenga ofa ya euro milioni 45 kumsajili mchezaji huyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
DRINKWATER ASHINIKIZA KUTUA CHELSEA
Mshindi wa taji la Ligi Kuu Uingereza Danny Drinkwater amejipanga kuiambia Leicester City kuwa anataka kutimkia Chelsea, Mirror limeripoti.
CHELSEA WANAMTAKA AURIER
Antonio Conte anataka kumsajili beki wa PSG Serge Aurier kwenye timu ya Chelsea ikiwa Mwaivory Coast huyo atafunguliwa viza kuingia Uingereza, Telegraph limeripoti.
Muitaliano huyo anataka kumpa changamoto ya ushindani Marcos Alonso na Victor Moses, kadhalika Ross Barkley, Antonio Candreva na Alex Oxlade-Chamberlain wapo kwenye rada za Chelsea.
HAZARD ASHINIKIZA KUTUA MADRID
Eden Hazard yupo tayari kushinikiza kuondoka Chelsea kwa sababu anataka kutimiza ndoto yake kuichezea klabu ya Real Madrid, limeripoti Don Balon .
CITY YAMUULIZIA BUSQUETS
Manchester City imeulizia uwezekano wa kumsajili beki wa Barcelona Sergio Busquets, kwa mujibu wa Onda Cero .
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia amecheza kipindi chote Camp Nou tangu alipoanza kucheza soka, na katika kipindi hicho pia alifurahia kucheza chini ya Pep Guardiola ambaye ni kocha wa sasa wa Manchester City.
PSG YAMTENGEA MBAPPE DAU NONO
Paris Saint-Germain wapo tayari kumsajli Kylian Mbappe kutoka Monaco kuungana na mchezaji waliyemsajli kwa dau la rekodi ya dunia Neymar, kwa mujibu wa Le Parisien .
Miamba hao wa Ufaransa wamejipanga kutumia kiasi cha £161 millioni kwa ajili ya kinda huyo mwenye kipaji cha hali ya juu, kuizima Real Madrid na Manchester City zinazoinyemelea saini ya kinda huyo, wanaweza kumuuza Angel Di Maria kuongeza fedha za ununuzi huo.
BARCELONA YAMFUKUZIA LEMAR...
Barcelona imeingia kwenye mbio za kumfukuzia winga wa Monaco Thomas Lemar, L'Equipe kimeripoti.
Baada ya kumuuza Neymar, miamba wa Catalans wanaamini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa atakuwa mabadala wake sahihi, na wanaongoza mbio za kumwania mchezaji huyo anayecheza upande wa kushoto.
Arsenal tayari wameshatoa ofa tatu ambazo zilikataliwa, Manchester City na Liverpool nazo zinatamani huduma yake.
... NA WANAKAZA MWENDO KUMPATA DEMBELE
Barcelona wamepiga hatua katika mbio za kumsajili Ousmane Dembele kutoka Borussia Dortmund baada ya Neymar kutimkia PSG kwa mujibu wa L 'Equipe .
BALE ANATAKA KUTIMKIA UNITED
Gareth Bale amemwambia mchezaji mwenzake wa Real Madrid Luka Modric kwamba anataka kurudi Ligi Kuu Uingereza kujiunga na Manchester United limeripoti Don Balon .
DRINKWATER YU TAYARI KUTUA CHELSEA
Danny Drinkwater wa Leicester City yupo tayari kuiambia klabu hiyo kwamba anataka kujiunga na Chelsea, kwa mujibu wa Mirror .
MONACO YATENGA £45M KUMSAJILI ALEXIS
Monaco wanataka kujiimarisha zaidi dirisha la uhamisho wa majira ya joto na wameandaa paundi milioni 45 kwa ajili ya Alexis Sanchez wa Arsenal, kwa mujibu wa The Sun .
CHELSEA YAMWANDALIA £50M VAN DIJK
Chelsea wamejipanga kutoa ofa ya paundi milioni 50 kwa ajili ya beki wa Southampton Virgil van Dijk, kwa mujibu wa The Times .
PALACE YAMGEUKIA FOSU-MENSAH
Crystal Palace wanajipanga kumsajili beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah kwa mkataba wa mkopo kipindi cha msimu mmoja, kwa mujibu wa The Sun .
Post a Comment