UPINZANI KENYA WATAKA RAILA ATANGAZWE RAIS
Upinzani Kenya unaamini mgombea wake Raila Odinga
ameshinda urais, ukikataa matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume ya
Uchaguzi IEBC yanayomuonesha Rais Uhuru Kenyatta akiongoza katika
uchaguzi uliokuwa na mashaka.
Awali waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry,
anayeongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi katika kituo cha Carter,
alisema ana imani na mfumo wa kielektroniki uliotumika katika uchaguzi
wa Kenya. Zaidi ya waangalizi 400 wa kimataifa walishuhudia uchaguzi huo
wa Jumanne iliyopita.
Hata hivyo upinzani unaedelea kudai kwamba uhesabuji wa kura ulikuwa wa udanganyifu baada ya Odinga kusema Jumatano kwamba mtambo wa kielektroniki wa kupigia kura ulidukuliwa na matokeo yalifanyiwa ukarabati. Tume ya IEBC inaendelea kusisitiza kwamba mtambo wake wa kielektroniki wa kupiga kura haujaathiriwa, licha ya majaribio dhahiri ya kutaka kufanya hivyo.

Post a Comment