MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MPELA KATA YA IPUNGA WILAYANI MBOZI MKOANI SOGWE SUBATI MKONDYA AMEPEWA MUDA WA MIEZI MIWILI KUWEZA KUKAMILISHA UJENZI WA MACHINJIO YA NYAMA
Wakizungumza mbele ya
Mbunge wa Vwawa Japhet Hasunga alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika Kijiji
hicho baadhi ya wananchi Rusayo Mtafya pamoja na John Siame wamesema kuwa kwa
kipindi kirefu kijiji hicho hakikuwa na sehemu ya kuchinjia nyama na kuwaweka
wananchi hao katika hali ya hatari kutokana na kula nyama ambazo zinachinjwa
sehemu si salama.
Haji Hamisi Ibrahimu
Afisa Tarafa wa Vwawa amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo katika Kata ya Ipunga
ambapo aliamua kumpa Mwenyekiti wa Kijiji hicho muda wa Miezi Miwli kuweza
kujenga na kukamilisha Ujenzi wa Machinjio hiyo.
Kwa upande wa
Mwenyekiti huyo Subati Mkondya amekiri kupokea agizo hilo la Afisa Tarafa ya
Vwawa na kuahidi kulitekeleza kwa muda aliopangiwa lakini pia amewaomba
Viongozi waweze kumsaidia katika kukamilisha ujenzi huo kwani peke yake
hatoweza.
Naye Mbunge wa Vwawa
Japhet Hasunga ameahidi kusimamia na kufanyia kazi mchakato huo wa ujenzi wa
Machinjio hayo haraka iwezekanyo ili kutatua tatizo la kula nyama ambazo zinachinjwa onyo kwani
kufanya hivyo ni hatari kwa afya za Binadamu.
Post a Comment