MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) NYANDA ZA JUU KUSINI WAMETOA ELIMU ZAIDI JUU YA HUDUMA YA MAWASILIANO YA KIMTANDAO KWA NJIA YA SIMU (MNP) INAYOMUWEZESHA MWANANCHI KUHAMA MTANDAO MMOJA KWENDA MTANDAO MWINGINE BILA KUBADILI NAMBA YA SIMU.
MBEYA
Huduma hiyo ya MOBILE NUMBER PORTABILITY (MNP)
ambayo imeanzishwa rasimi mwezi march mwaka huu na mamlaka hiyo ni huduma ya
hiari itakayompa uhuru mwananchi kuweza kuhama mtandao wowote wa simu anaotaka
na kuendelea kupata mawasiliano bila kulazimika kubadili namba yake ya simu.
Akitoa ufafanuzi wa namna ya matumizi ya huduma hiyo
katika kikao kilichowakutanisha na waandishi wa habari katika ofisi za mamlaka
hiyo jijini mbeya mhandisi eng MWESINGWA FELISIAN amesema ili kuweza
kufanikisha huduma hiyo ni lazima kufuata taratibu na sheria zilizowekwa ikiwa
ni pamoja na kumtafuta mtoa huduma mwenye ubunifu na huduma zake.
Mwesingwa ameongeza kuwa lengo la kuleta huduma hiyo
kwa wananchi ni kuongeza ushindani kwenye sekta ya mawasiliano ambayo
itachochea utoaji huduma bora na zenye gharama nafuu na kwamba kama kutakuwa na
mtandao ambao huduma zake haziridhishi basi wateja watahama mtandao huo na
kuhamia mtandao mwingine pasipo na usumbufu wowote.
Aidha amessisitiza ili kuweza kupata huduma hiyo
mwananchi atatakiwa kutuma ujumbe mfupi SMS wenye neno HAMA au PORT kwenda
namba 15080 ambayo ni namba maalumu ya kuhama na hii ni katika kudhibiti
udanganyifu na endapo kutakua na kiasi chochote cha pesa kwenye line mwananchi
atatakiwa kukitoa kwanza ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi
wa habari ikiwemo baadhi ya mitandao ya simu huduma zake kuwa kero kwa wananchi
hususani mawasiliano kutokupatikana muda wote ikiwa ni pamoja na wananchi wanaoishi
vijijini ambapo mara nyingi mtandao huwa ni shida, naibu mkurugenzi msaidizi
maswala ya malalamiko THADAYO RINGO amesema swala hilo bado linafanyiwa ufumbuzi
na kwamba muda wowote hizo kero zitakwisha.
Post a Comment