LIGI KUU NCHINI UINGELEZA KUANZA LEO USIKU KWA ARSENAL KUWAKARIBISHA LEICESTER CITY
Ligi Kuu Uingereza itaanza rasmi Ijumaa usiku kwa mara ya kwanza tena Arsenal na Leicester City zitakaposhuka dimbani, mubashara
Vijana wa Arsene Wenger walimaliza nje ya nne bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu 1996.
Hata hivyo, Wenger alipunguza machungu kwa kutwaa kombe la FA katika uwanja wa Wembley na anaanza kampeni za msimu huu akiwa amesaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Arsenal watataka kuanza vema msimu huu tofauti na misimu ya miaka ya hivi karibuni waliyoanza kwa vipigo. Gunners wameshinda mechi moja tu kati ya saba za mechi za ufunguzi wa ligi, wakichezea kichapo mechi tatu kati ya nne za mwisho.
Kwa upande mwingine, Leicester, ambao wanaanza kampeni kwa mara ya kwanza chini ya Craig Shakespeare, wamecheza mechi 21 bila kushinda dhidi ya Arsenal katika Ligi Kuu Uingereza (Sare 7 na vichapo 14), ushindi wao pekee dhidi ya Gunners ukiwa mechi yao ya kwanza Ligi Kuu Novemba 1994.
Matarajio baina ya klabu mbili yanatofautiana, lakini presha inalingana baina ya mameneja wote ambao wote wanataka matokeo mazuri msimu huu.
Mechi | Arsenal vs Leicester City |
Tarehe | Ijumaa Agosti 11 |
Muda | 21:45 saa za Afrika Mashariki |
Katika Tanzania mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Uingereza itarushwa Mubashara kupitia televisheni ya Super Sport kadhalika mtandaoni kupitia Sky Go.
VIKOSI & HABARI ZA TIMU
Arsene Wenger amethibitisha kuwa Alexis Sanchez hatakuwepo kwenye kikosi chake kitakachocheza mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Uingereza baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile kupata maumivu ya misuli ya tumbo mazoezini.
Kuna hofu pia juu ya uzima wa Mesut Ozil na Aaron Ramsey, na Per Mertesacker pia hapana uhakika baada ya kulazimika kutoka dimbani Jumapili iliyopita mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea.
Laurent Koscielny anatumikia adhabu, lakini Shkodran Mustafi anaweza kushuka dimbani ikiwa Wenger anaamini mchezaji huyo yupo tayari.
Kikosi cha Kwanza Arsenal: Cech; Holding, Mertesacker/Mustafi, Monreal; Bellerin, Elneny, Xhaka, Kolasinac; Walcott, Lacazette, Iwobi
Robert Huth hatacheza dhidi ya Arsenal kwani bado anaendelea kuuguza majeraha yake ya kifundo cha mguu, wakati Danny Drinkwater pia yu shakani kutocheza kutokana na majeraha lakini Islam Slimani atacheza baada ya kupona majeraha aliyopata kipindi cha maandalizi ya msimu.
Kelechi Iheanacho atakuwepo kwenye kikosi cha Shakeaspere kushirikiana na Jamie Vardy katika safu ya mashambulizi.
Potential Leicester XI: Schmeichel; Simpson, Morgan, Maguire, Fuchs; Albrighton, James, Ndidi, Gray; Vardy, Iheanacho.
Post a Comment