MILIONI 15 ZA UJENZI WA BARABARA SONGWE ZAZUA UTATA,MRADI WATELEKEZWA WANANCHI WAPAGAWA.
MKWAJUNI-SONGWE
FEDHA milioni 15 zilizotolewa na
serikali kwa ajili ya ujenzi wa awali wa barabara ya kiwango cha vumbi kilometa
10 katika barabara zilizopo kata ya Ifwenkenya halmashauri ya Mkwajuni wilayani
Songwe mkoani Songwe zazua utata baada ya mradi wa ujenzi huo kutelekezwa muda
mchache baada ya kuanza utekelezaji.
Hatua hiyo imejitokeza mwishoni mwa
wiki kwenye mkutano wa hadhara wa viongozi wa halmashauri hiyo walipokuwa
wakizungumza na wananchi wa vijiji vilivyopo kata ya Ifwenkenya,baada ya kuwepo
kwa changamoto nyingi za kiutendaji ambapo wananchi walitoa ya moyoni ikiwemo
kutelekezwa kwa mradi.
Jimmy Melimeli mkazi wa
Ifwenkenya,alisema walitangaziwa kuwa fedha za awali milioni 15 za ujenzi wa
barabara ya kiwango cha vumbi zimefika na ujenzi ulianza lakini haikumaliza
hata wiki moja wakashangaa kuona mradi huo umetelekezwa pasipo kupewa taarifa
yeyote kuhusu sababu ya kukwama kwake.
Vicent Mpanzo,afisa mtendaji wa kata
hiyo,alisema baada ya kukwama mradi huo alifuatwa na baadhi ya wananchi
wakihoji tatizo la kukwama amapo alisema hakuwa na majibu na baada ya hapo
alipeleka tarifa halmashauri ya wilaya ambao wamekuja kuzungumzia suala hilo
kupitia mkutano wa hadhara.
Akizungumza sababu ya kukwama kwa
mradi huo,baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya hiyo,injinia wa ujenzi wilayani Songwe,Ernest Mgeni,alisema tatizo ni
uhaba wa maji kutokana na eneo hilo kuwa na vumbi nyingi,na kwamba tatizo la
kuharibika kwa barabara hizo ni magari makubwa ambayo tani zake haziruhusu
kupita.
Alisema kwa sasa suala hilo lipo
kwenye chombo kipya kulicho anzishwa na Rais Magufuli kiitwacho Talura kuwa
ndicho kitakachosimamia ujenzi wa barabara zote za halmashauri ambapo fedha
zote za ujenzi zitapelekwa huko,kauli ambayo ilipingwa vikali na wananchi
katika mkutano huo.
Wananchi walihoji kuwa kama tatizo
ni maji,kwanini wasijenge barabara hizo mwezi wa nne kipindi cha mvua ambapo
maji yanakuwa mengi?na kwamba maeneo yote ya kata hiyo yamekuwa na vumbi nyingi
hali inayosababisha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza.
Hata hivyo,mwenyekiti wa halmashauri
hiyo,Abraham Sambila aliingilia kati na kusema kuwa mkakati wa kujenga barabara
za kata hizo ulikuwa kilometa 25 kwa kuanzia ujenzi ni kilometa 10,baada ya
kukwama kwa mradi huo,ni kutokana na madai ya ukosefu wa maji kuitokana na
kuwepo kwa vumbi nyingi.
Alisema hayo ndiyo majibu waliyopewa
na wataalam katika vikao vyao na ndiyo maana katika mkutano huo wamewaleta
mbele ya wananchi ili wajibu,na kwamba kwa sasa hawatashiriki tena ujenzi huo
kutokana na kuhasisiwa chombo kipya Tarula,kitakacho simamia shughuri zote za
barabara za halmashauri na kuwataka wananchi kuwa watulivu,wakati utekelezaji
unaanza.
Post a Comment