MWENYEKITI WA KIJIJI MBARONI AKITUHUMIWA KUWATOZA FAINI WASUKUMA PASIPO KUWAPA LISITI,FEDHA HIZO HUFANYIA UFUSKA NA WAKE ZA WATU.
MOMBA-SONGWE
MWENYEKITI wa kijiji cha Senga
wilayani Momba mkoani Songwe,Ernes Malocha (CCM) amekamatwa na kutiwa mbaroni
na jeshi la polisi tarafa ya Kamsamba,akituhumiwa kuwatoza fedha kandamizi
wafugaji jamii ya wasukuma wa bonde la Kamsamba pasipo kuwapa lisiti,kasha
fedha hizo kutumia kwa ufuska.
Hatua hiyo imekuja siku za hivi
karibuni baada ya kuwepo kwa malalamiko miungoni mwa wafugaji kuwa mwenyekiti
huyo amewageuza kuwa mradi wa kujipatia kipato kwa kuwatoza faini kubwa mara
kwa mara pasipo kuwapa lisiti huku fedha hizo akizitumia kwa anasa za ulevi na
kuwarubuni wake za watu.
Jofrey kalincho mfugaji,alisema juzi
kijana wake alienda kunywesha maji eneo tengefu mto Momba,lakini alisikitishwa
kusikia kijana wake alipigwa na kuumizwa vibaya na mwenyekiti huyo na
alipofuatilia aliona ng’ombe zake zaidi ya 100 zimekamatwa zikidaiwa kuingia
eneo lisilo rasmi kunywa maji.
Alisema alipo hoji zaidi aliambiwa
na mwenyekiti huyo,akiwa na afisa mifugo wa bonde hilo,Titto Ndegela kuwa alipe
faini ya milioni moja vinginevyo mifugo yake itapigwa mnada,ambapo alilaimika
kujitetea na kulipa fedha pungufu ya milioni moja kasha kupewa mifugo yake.
Aliongeza kuwa ilipofika jioni
alishangaa kuona mwenyekiti huyo akila starehe kwa kunywa pombe na nyama choma
akiwa na wake za watu kwenye virabu tofauti tofauti,na kuanza kujiuliza ambapo
alipata wazo kutoka kwa msamalia mmoja kuwa akadai lisiti na pia aende polisi
kutoa taarifa.
Alisema alipofika polisi mwenyekiti
huyo aliitwa polisi na ilipobainika kuwa mwandishi wa gazeti hili yupo
kufuatilia tukio hilo,ndipo alipowekwa lumande kabla ya kuwekewa dhamana na
baadhi ya viongozi wenzake na kutakiwa kughalamia matibabu ya kijana wake
aliyepigwa na kulazwa hospitali ya Misheni.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri hiyo,Emelye Mfugale,alisema amepata taarifa kupitia kwa afisa
tarafa wa bonde hilo,na kwamba kutokana na mwenyekiti huyo kutoza fedha nyingi
pasipo kuwapa lisiti wafugaji hao,alisema hakunafedha iliyowahi kuletwa katika
halmashauri ya Momba.
Methew Chikoti,alisema kutokana na
kuwepo kwa vitendo hivyo,halmashauri italazimika kwenda kufanya mikutano ya
hadhara kwenye maeneo hayo ili wafugaji wafundishwe sheria za malipo ikiwemo
kuwafunda wenyeviti wanaotumia mwanya wa kuwatisha wafugaji ili wapate fedha
ambazo hata hivyo haziingii kwenye kapu la halmashauri.
Mkuu wa wilaya Momba Juma
Irando,alisema alikwisha wakataza wenyeviti wa vijiji kuhusika kwenye malipo ya
aina yeyote,lakini kumekuwepo na hali ya dharau kwa baadhi ya wenyeviti na hata
kufikia hatua ya kuwaingiza wafugaji kinyemela na kuchukua fedha zao bila
kujali kuwa wanaharibu mazingira.
Alisema kwa sasa atageuka mboga kwa
kuwashughurikia wenyeviti wanao kaidi maagizo ya serikali na hata kuwachukulia
hatua wanaokusanya fedha kinyemela kwa wafugaji pasipo kuwapa lisiti huku
wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Post a Comment