Header Ads


YANGA YASHUSHA KIFAA KIMYA KIMYA

 KOCHA wa Yanga, George Lwandamina anarejea nchini kesho Jumatano, lakini timu hiyo imemshusha kimyakimya Dar es Salaam, nahodha wa timu Cameroon ya wachezaji wa ndani, Fenando Bongnyang.
Staa huyo anayeichezea Cotton Sports ametua akiwa mchezaji huru kwa maelezo kwamba mkataba wake umemalizika na ameletwa na mmoja wa mawakala wa Yanga ingawa Mwanaspoti limeambiwa kuwa kocha amesisitiza kisifanyike chochote mpaka afike.
Faili la mchezaji huyo linaonyesha kwamba amekulia kwenye akademi mbalimbali na sifa yake kubwa kwa mujibu wa magazeti ya Cameroon ni mpaka rangi kwenye kiungo na mchezaji mwenye sifa ya kuchezesha timu na kupiga pasi za kupenyeza.

Staa huyo inaelezwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kukaba lakini Mwanaspoti linajua kwamba tayari Lwandamina kwenye faili lake ana majina mawili ambayo ni Kabamba Tshishimbi aliyekuwa akimuangalia
nchini Swaziland juzi Jumapili na Cletius Chota Chama wa Zambia.
Habari zinasema kwamba viongozi wa Yanga wameangalia uwezo wa mchezaji huyo kupitia video na rekodi zake wakafurahia ingawa hawana mamlaka yoyote juu ya Lwandamina.
Rekodi za mchezaji huyo ambaye Yanga wanamfanya siri kubwa zinaonyesha kwamba amekuwa tegemeo kubwa kwa timu ya Taifa ya Cameroon ya wachezaji wa ndani na aliwahi kupata dili kadhaa akatoka nje lakini akarudi.

Yanga wamekuwa wakifanya ujio huo siri kwa kuhofia kufanyiwa fujo na watani zao kutokana na kiburi cha fedha ya mfadhili wao, Mohammed Dewji ‘Mo’.
Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Yanga mwenye ushawishi kwenye kamati ya usajili ni kuwa ujio wake kama ukibarikiwa na kocha utafuta nyayo za Haruna Niyonzima ambaye ameibukia Simba licha ya kwamba hawajamtangaza.
Pia inahalalisha Yanga kuachana rasmi na Mkata Umeme ambaye alishindwa kuonyesha makeke katika kipindi chote alichokuwa
Jangwani.    

No comments

Powered by Blogger.