WANAUME KUANZIA MIAKA 10 MKOANI SONGWE WAMETAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUFANYA TOHALA
SONGWE -Tunduma
Na manuel kaminyoge
Wanaume wote kuanzia umri wa miaka kumi na kuendelea mkoani songwe wametakiwa kujitokez kwa wingi kufanyiwa huduma ya
tohara inayo tolewa katika vituo 8 mkoani hapa kwa lengo la kupunguza
maambukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa mengine . Na manuel kaminyoge
Wito huo
umetolewa na mkuu wa wilaya ya momba
juma saidi irando kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa songwe wakati wa ufunguzi wa
utoaji huduma ya tohala mkoani songwe uliofanyika katika viwanja vya shule ya
msingi mwaka tunduma wilayani momba mkoani hapa.
Irando
amesema kuwa licha ya kuwa kila kabila lina mila na desturi zake wanaume
wasifanye kigezo cha kutofanyiwa tohara kwani tohara hupunguza maambukizi ya
virusi vya ukimwi kwa 60% na kusaidia
kumuokoa mama na magonjwa kama salatani ya shingo ya kizazi.
Mmoja wa
watoa huduma neema eliasi wmesema kuwa wanakumbana na changamoto nyingi katika
zoezi la tohala ya mwanaume kwani baadhi yao wanaogopa kufanya tohara huku
wengine wakivizia usiku ili wasionekane wanapoenda kufanya tohala .
Neema
ameongeza kuwa kuna baadhi ya wanaume huwa wanaamini mambo ya ushilikina na
kutaka baada ya kufanyiwa wapewe ngozi yao iliyokatwa na kusema kuwa wanataka
wakazike ngozi hizo zilizokatwa.
Innocent
ndunguru mratibu tohara mkoa wa songwe wakati akisoma lisala amesema kuwa
kwenye zoezi hili wamekuwa wakikumbana na chanagamoto mbalimbali ikiwa ni
pamoja na upungufu wa vifaa kama vitanda na kuiomba serikali iwasaidie licha
kuwa mpaka sasa wamevuka lengo walilokuwa wamejiwekea kwa kufikia zaidi ya 80%
.
Contact 0762306521 / mwabhulye93@gmail.com
Post a Comment