WANANCHI WA KIJIJI CHA IDIBILA KATA YA LUANDA MKOANI SONGWE WAMEZITAJA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO KIJIJINI HAPO
Wakizungumza katika
Mkutano wa hadhara uliofanywa jana kijijini hapo kwa lengo la kutoa kero zao
mbele ya Mbunge wa jimbo la Vwawa Japhet
Hasanga wananchi hao wamesema tatizo la maji limekuwa sugu kwao jambo
linalowafanya kunywa maji ambayo siyo safi kwa afya hivyo wamemwomba Mbunge
huyo kuwasaidia katika suala hilo.
Kwa upande wa Wananchi
wa kijiji hicho Boniface Kanyela pamoja na Mikaeli Daimuni wamekiri kuwepo kwa
tatizo hilo na kuongeza kuwa changamoto nyingine wanayokabilianan nayo ni
ukosefu wa Barabara jambo linalolazimu wananchi hao kushindwa kufanya Shughuli
za Maendeleo kwani inawalazimu kutembea umbali mrefu kwa Miguu kufata mahitaji
yao pamoja na kukosekana Kivuko toka Ng’ambo moja kwenda nyingine pamoja na
kijiji hicho kuitwa kisiwa kutokana na ukavu uliopo katika maeneo hayo ya kata
ya Luanda.
Naye Mbunge wa Vwawa
Japhet Hasanga amesema kuwa amezipokea kero hizo za Wananchi hao na kuwaahidi
kuwa jambo hilo litatekelezwa mapema iwezekanavyo.
Post a Comment