MWANAMKE MMOJA MKAZI WA MWANSHINGA JIJINI MBEYA NA WANAWE WAWILI, WAMEMWAGIWA MAJI YANAYOSADIKIWA KUWA TINDIKALI
MBEYA
Akizungumza jana
akiwa amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Sankemwa amesema tukio hilo
limetokea saa 3:30 usiku wa Julai 19, eneo la Malema, Mwanjelwa wakati mwanamke
huyo, Vumilia Sankemwa (31), akiwa njiani kurejea nyumbani.
Amewataja watoto
aliokuwa nao kuwa ni Loveness Peter (11), ambaye ni mwanafunzi wa darasa la
sita wa Shule ya Msingi Sinde ambaye amejeruhiwa usoni na mwilini na Nancy
Peter (5 ambaye ametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.).
Daktari wa zamu
hospitalini hapo, Margaret Kimwaga amesema wamempokea mgonjwa huyo akiwa na
hali mbaya, lakini sasa anaendelea vizuri.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema ofisi yake ilikuwa haina taarifa
ya tukio hilo hadi jana asubuhi na wameanza kulifanyia kazi.
Post a Comment