MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATEMBELEA HOSPITALI YA AMANA
Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi
wa wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayoendelea kujengwa Hospital
ya rufaa ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi
huo umekamilika kwa 100%.
Jitihada hizo zimefanywa na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Paul Makonda ambae kwa kiasi kikubwa amekuwa chachu ya
maendeleo makubwa katika sekta ya afya katika mkoa wake.
Ikumbukwe tu katika jitihada za
maendeleo ya idara ya afya zinazofanywa na mkuu huyo, ambapo tarehe 11
mwezi Julai mwaka huu alizindua jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la
huduma za dharula katika hospitali ya Temeke ikiwa ni mwendelezo wa
kuhakikisha mkoa huo unaondokana na matatizo ama changamoto za afya.
Awali hospitali ya Mwananyamala ,na
Amana zilikuwa na malalamiko mengi ikwemo wagonjwa kudai kutopata huduma
ya uhakika, lakini Mkuu wa mkoa huyo amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa
Dar es salaam kuwa wao kama serikali wanaendeleza jitihada ya
kuhakikisha mazingira ya utoaji huduma za afya katika hospitali hizo
zinaimarika kwa kiasi kikubwa.
Huu ni muonekano wa jengo la zamani la kutolea huduma za akina mama na watoto. |
Wodi hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa
kuchukuwa vitanda 150 sambamba na Vifaa kisasa vya kutolea huduma,
Vyumba vya Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na
sehemu ya kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.
Muonekano ya wodi mpya ya wazazi na watoto ikiwa ipo katika hatua za mwisho kukamilika. |
Ujenzi huo unafadhiliwa na Kampuni tanzu
ya Mafuta na Saruji ya Amsons Group ambayo imekubali kumuunga mkono
Mheshimiwa Makonda kwa kujenga wodi tatu wazazi na watoto kwenye
Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala ambapo zote zitakuwa na uwezo
wa kuchukuwa vitanda 450.
Muonekano wa jengo jipya la kutolea huduma za akina mama na watoto katika hospitali ya rufaa ya amana jiji Dar es salaam. |
“Ujenzi huu na hatua iliyofikia inatoa
matumaini mapya kwa kinamama, watoto na wakazi wa Dar es salaam juu ya
upatikanaji wa huduma bora na nzuri kwenye Hospital zetu za
Serikali,watu walishazoea huduma nzuri zinapatikana nje ya Hospital za
Serikali lakini kwa sasa hali itabadilika, na nina uhakika ndani ya muda
mfupi tutamuomba Rais Dr.Magufuli aje atuzindulie hizi wodi kama
ishara ya kumbukumbu ya kazi aliyoianza alipotembelea Hospital ya
Muhimbili na kukuta watu wamelala chini na kutafuta majibu, sisi
wasaidizi wake ametupa kazi ya kutatua kero za wananchi, hivi ndivyo
tunavyozitatua kwa vitendo” Alisema.
Aidha Makonda amesema wodi hiyo
itazidisha upatikanaji mzuri wa huduma bora za Afya kwa wakazi wa jiji
la Dar es salaam huku akieleza kuwa lengo lake ni kuhakikisha Dar es
Salaam inakuwa mkoa unaotoa huduma bora za Afya.
“Kama mnakumbuka wakati tunakuja wodi
iliyokuwa ikitumik akinamama walikuwa wakilundikana chini na wengine
wanatumia kitanda kimoja zaidi ya watatu hadi wanne na wakati mwingine
walikuwa wakilazimika kurudi nyumbani kabla ya muda wa madaktari
kuruhusu kutokana na mazingira duni yaliyokuwa yakikabili wodi hiyo,
lakini wodi hii itamaliza kero hiyo” Aliongeza Makonda.
Mkuu wa mkoa Dar e salaam Paul Makonda (wapili kushoto) akizungumza na Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya amana. |
Hata hivyo Makonda amewataka wadau wa
maendeleo wenye dhamira ya kuchangia shughuli za Maendeleo kwenye Mkoa
wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi Ofisini kwake na Ofisi za Wilaya
kuungana na Serikali kuujenga Mkoa huo.
“Nawapongeza watumishi na wafanyakazi wa
Afya kwenye Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala kwa kazi kubwa
wanayoifanya kupunguza kero kwenye Sekta ya Afya” Alisema Makonda.
Post a Comment