Misa ya wafu ya mwendazake Nkaiserry kufanyika leo
KENYA
Misa ya wafu kwa ajili ya mwendazake aliyekuwa waziri wa masuala ya ndani Jospeh Nkaiserry itaandaliwa alasiri ya leo. Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanatarajiwa kuwa miongoni mwa watakaohudhuria misa hiyo. Kamati mandaalizi ya mazishi ya Nkaissery inasema matayarisho yote yamekamilika. Mweyekiti wa kamati hiyo waziri Cleopa Mailu anasema mwili wake Nkaissery baadaye utasafirishwa hadi nyumbani kwake Ilibisil Kajiado, ambako atazikwa Jumamosi hii.
Post a Comment