IEBC yalaani visa vya kuvurugwa kwa mikutano ya kisiasa
KENYA
Tume ya uchaguzi IEBC imelaani visa vya kuvurugwa mikutano ya kisiasa katika maeneo mbali mbali nchini. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewataka wananchi kuwaruhusu viongozi kuuza sera zao katika maeneo yao bila kuvuruga mikutano yao. Kauli yake inajiri kufuatia visa ambapo naibu rais William Ruto na viongozi wa NASA walizomewa na kulazimika kutatiza hotuba zao katika kaunti za Kisumu na Baringo mtawalia
Post a Comment