WANANCHI WA CHUNYA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA KWA KUKOSA MAJI SAFI NA SALAMA
Mbozi -songwe
Na manuel kaminyoge
Mahakama ya mwanzo vwawa mjini
imempandisha kizimbani lotali westoni (35) mkazi wa kijiji cha Luanda kilichopo
tarafa ya vwawa wilaya ya mbozi mkoani songwe kwa shitaka la kupatikana na pombe
ya moshi/ gongo pamoja na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo kinyume na kifungu
cha sheria 62 na 30 kanuni ya adhabu sura
ya 16 .
Akisomewa shitaka
hilo mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi doni pita mbele
ya hakimu wa mahakama hiyo Christina mlwilo amesema kuwa mshitakiwa alitenda kosa
hilo julai 13 mwaka huu saa 3 asubuhi huko
katika kijiji cha luwanda .
Pita ameongeza
kuwa mshitakiwa alikutwa na pombe ya moshi/ gongo pamoja na mitambo ambayo ndiyo alikuwa akitumia kutengenezea pombe hiyo haramu huku
akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume cha sheria .
Aidha mshitakiwa
amekili kutenda kosa hilo na hakimu wa mahakama hiyo Christina mlwilo
ameahilisha shauri hilo mpaka julai 17
mwaka huu ilitakaposikilizwa tena na mshitakiwa amepelekwa mahabusu.
Wakati huohuo
Susana mtindo (30) mkazi wa eneo hilohilo naye amepandishwa kizimbani katika
mahakama ya mwanzo kwa shitaka la kupatikana na gonngo pamoja na mitambo ya
kutengenezea ambapo amekili kutenda kosa hilo na hakimu wa mahakama hiyo matha
malima ameahilisha shauri hilo mpaka julai 13 na mshitakiwa amepelekwa lumande.
Songwe
Asilimia 70 ya wakazi wa wilaya ya
songwe mkoani songwe wanaugua homa za
matumbo kwa kunywa maji yasiyo safi na salama na wakiyafuata maji hayo umbali
wa kilometa 30 licha ya kuwa si salama kwa kunywa ambapo dumu moja hununuliwa
kwa sh 300.
Hayo yamesemwa
dakitari wa hospitali ya mwambani fransisi mwalugala ambapo amesema kuwa majia
ni changamoto kubwa kwa utoaji huduma katika hospitali hiyo kutokana na
wagonjwa wengi kuumwa homa ya matumbo ambapo chanzo ni uhaba wa maji wilayani
humo.
Baadhi ya wananchi
wa mkwajuni wilayani humo magreti selemani na Beatrice mkoko wamesema kuwa ndoa zao zipo kuachika kwa
sababu ya maji kwani wamekuwa wakiamka usiku kufuata maji na kuwaacha waume zao
wamelala kitu ambacho ni hatali kwa familia zao na jamiii kwa ujumla .
Wananchi hao
wameongeza kuwa shughuli nyingi zinakwama kwa sababu ya maji na kuiomba
serekali iwaangalie wananchi wa wilaya ya songwe waangaliwe kwa jicho la
huruma.
Mhandisi wa
wilaya ya songwe ndele mengo amesema kuwa wamefanya jitihada mbalimbali za
kuwasiliana na idala mbalimbali ikiwepo wizala ya maji nakuomba kujenga mladi
mpya mkwajuni na ombi hilo limepokelewa na linashughulikiwa.
Filipo mlugo
mbunge wa jimbo la songwe amekili kuwepo tatizo hilo kwenye jimbo lake lakini
ameshukuru serikali ya awamu ya tano kwa mwaka huu wa fedha kwenye bajeti suala hilo limewekwa na kwamba fedha zikiwa
tayari atapewa kwa ajili ya suara la maji.
Mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya songwe
samweli nawela amesema kuwa kama halimashauri wameona ziwa lukwa ndo itakuwa
suluhisho kwa tatizo hilo kwa kizazi hiki na kijacho na kwamba kwenye bajeti limeingizwa na hatua za mwanzo
zimeanza kuchukuliwa contact 0762306521/ mwabhulye93@gmail.com
Post a Comment