KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KULAWITI
Momba-SONGWE
Na manuel kaminyoge
MAHAKAMA ya wilaya ya Momba mkoani Songwe imemhukumu
kutumikia kifungo cha maisha kijana aliyejulikana kwa jina la Duma Lundilo
Pangarasi, mkazi wa Isanzo Chunya mkoani Mbeya kwa kosa la Kubaka na kulawiti
mtoto wa kiume mwanafunzi wa darasa la tatu
wa shule ya msingi Mbao iliyopo Wilayani Momba.
Duma Ludilo
Pangarasi mwenye miaka 26, alikuwa akikabiliwa nakesi ya jinai namba 196 /
2016, shauri ambalo lilifikishwa mahakamani hapo mnamo Novemba 8 /2016 Mbele ya hakimu Mfawidhi Zabibu Mpangule akituhumiwa
kumlawiti mtoto huyo kinyume cha sheria
154/kifungu cha kwanza A na cha
pili kanuni ya adhabu sura 16 ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Ilielezwa
mahakakani hapo na mwendesha mashtaka wa
polisi Leonard Mwamafupa mbele ya hakimu
mkazi wa mahakama ya Wiaya James
Mhanusi kuwa shahidi wa kwanza ambaye ni mtoto aliyelalawitiwa
aliieleza mahakama kuwa mnamo Nove 7
2016 muda wa mchana akitoka shule
alichomwa na mwiba katika harakati za kuchomoa mwiba katika kiatu chake
alikurupushwa na mtu aliyetoa kichakani akiwa na fimbo mkononi na kumtaka asikimbie vinginevyo angemuua .
Baada ya
kusimama aliamuriwa kuvua nguo zote mtoto alitii na kisha Pangarasi alitekeleza
tendo hilo la kinyama na alipotosheka akamwacha aende zake, mtoto huyo
alipofika kwa mzazi wake alimweleza huku akimtaja mtuhumiwa kwa jina la msukuma
mchunga Ng’ombe alimfanyia machafu hayo.
Mbele ya
mahakama mshtakiwa aliwahi kuomboleza kuwa adhabu aliyopata gerezani imemtosha
kujifunza hivyo aachiwe kwani hawezi
rudia kutenda kosa kama hilo, kauri iliyoashiria ukiri wa shitaka, maombolezo
ambayo yameifanya mahakama kuridhishwa na mashahidi waliotoa ushahidi
mahakamani hapo akiwemo mzazi pamoja na daktari Stanrey Simbeye ambaye alipokea
mtoto huyo kwaajili ya matibabu.
Aidha kabla
ya kutoa adhabu hiyo Hakimu Mhanusi amemtaka mshtakiwa ajitete kwani mahakama
imemtia hatiani, ndipo mshtakiwa alipoiomba mahakama isimpasie adhabu kali
kwani yeye ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi lakini pia anafamilia
inayomtegemea ombolezo ambalo limetupiliwa mbali na mahakama na kumhukumu
kutumikia kifungo cha maisha Jela ili iwe fundishisho kwa watu wengine.
contact 0762306521 /mwabhulye93@gmail.com
Post a Comment