MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA
Momba-songwe
na manuel kaminyoge
Aron Martin Silungwe mkazi wa
Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Songwe amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 Jela baada ya
kukutwa na hatia katika Kesi ya
Unyang’anyi wa Kutumia Silaha iliyokuwa ikimkabili katika mahakama Ya wilaya ya Momba.
Shauri hilo
jinai namba 93/217 lilifikishwa katika
mahakama ya Wilaya ya Momba Mnamo mei 9
mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi wa
Mahaka hiyo Mh.James Mhanus , ambapo mwendesha mashtaka wa Polisi Joery
Mori amesema mshtakiwa alikana shtaka na kusikilizwa pande mbili.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo Mnamo Mei 30 saa saba za
usiku katika Nyumba ya kulala wageni
ijulikanayo Super Time mali ya Mussa Ally ambaye ni shahidi namba moja,akaieleza mahakama kuwa mshtakiwa
na wenzake wawili wakiwa na silaha
mbalimbali Mapanga na
Nondo walifika katika nyumba yake
na kumteka mlinzi Haluna Msongole kisha kumfunga kamba na kumfungia chumba cha
Jiko Wakimtaka kunyamaza kimya endapo
angekaidi wangemuua, na kuvunja milango, walifanikiwa kuiba mali mbalimbali ikiwemo seti ya Muziki na Luninga zenye thamani ya zaidi ya
shilingii laki milioni 8 na pesa pesa za
mauzo ya siku.
Katika harakati
za kutekeleza tukio hilo, mmoja wa wageni aliyelala katika nyumba hiyo
alimpigia simu mmiliki wa Nyumba hiyo na kufanikiwa kuwahi kabla wezi hao
hawajaondoka eneo hilo wakiwa na usafiri wa pikipiki Aina ya Tibeter MC Yenye namba 309 BHD Mali ya Aron Godwin ambaye alikuwa
shahidi namba mbili katika shauri hilo, walijaribu kutoroka lakini mmiliki huyo
aliwagonga na gari na kusababisha ajali ambapo mshtakiwa na wenzake walitoroka
eneo hilo hadi alipokamatwa kwa mtego wa polisi kwa msaada wa mmiliki wa
pikipiki hiyo.
Shahidi namba mbili mmiliki wa pikipiki hiyo, aliiambia mahakama kuwa Mshtakiwa alikuwa na kawaida ya kuazima
pikipiki mara kwa mara na siku hiyo
aliazima akidai kuwa alikuwa na safari ya kijijini kwao kwa majukumu ya
kifamilia na kamba angeirudisha asubuhi badala yake siku ya tukio saa 9 za
usiku alimpigia simu akimueleza kuwa alikuwa ameporwa pikipiki na majambazi
alipotakiwa kuripoti kituo cha polisi hakuwa tayari na kumsihi yeye ambaye ni
mmliki aende polisi na sio yeye hadi alipotegewa mtego na kunasa mikononi mwa
sheria.
Akitoa
adhabu hiyo Hakimu Mhanusi amesema kosa launyang’anyi wa kutumia silaha ni
kinyume cha sheria namba 287 kifunguu
cha kwanza A cha kanuni ya adhabu namba 16 ya mwenendo wa makosa ya jinai
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, kutokana na wingi wa matukio ya mauaji na
ujambazi wa kutumia silaha Wilayani Momba Mwendesha mashtaka wa polisi akaiomba
mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa licha ya utetezi wake kuwa na familia
inayomtegemea hakimu mhanusi akatoa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 30
Jela ili kutoa funzo kwa wengine.
Post a Comment