NAIBU WAZIRI AELEZA UMUHENDA WA NISHATI KUWA AGENDA VIKAO VYA MAENDELEO
Naibu Waziri wa Nishati Subira
Mgalu akisisitza jambo wakati wa mkutano wake na wananchi wa kijiji cha
Itwangi Wilaya ya Shinyanga alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa
mradi wa REA.
Naibu Waziri wa Nishati Subira
Mgalu akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck
(katikati) alipomtembelea ofisini kwake wakati wa ziara yake mkoani
humo. Wanaofuatilia ni watendaji walioambatana na Naibu Waziri kutoka
Wizara ya Nishati, TANESCO na REA na Watumishi wa Mkoa wa Shinyanga.
Msimamizi wa Mradi wa REA Hussein
Shemdasi, (kulia) akimtambulisha Mkandarasi wa Mradi wa REA Mkoa wa
Shinyanga kutoka kampuni ya Angelic (kushoto).
Meneja wa Tanesco Kanda ya
Magharibi Macline Mbonile akieleza jambo wakati wa mkutano wa Naibu
Waziri na wananchi wa kijiji cha Itwangi.
Naibu Waziri wa Nishati Subira
Mgalu (kulia) akimweleza jambo Mku wa Wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro wakati Naibu Waziri alipomtembelea ofisini kwake.
………………….
Naibu Waziri wa Nishati Subira
Mgalu amewataka Wakuu wa Mikoa kuingiza Agenda ya Nishati katika
vikao vya Maendeleo vya mikoa kwa kuwa sekta hiyo ni kichocheo kikuu
cha sekta nyingine kiuchumi na kimaendeleo.
Aliyasema hayo wakati
alipomtebelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ofisini kwake wakati wa ziara ya
kukagua utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Nishati vijijini
unaotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) mkoani humo.
Aliongeza kuwa, ili sekta zote
ziweze kuendelea zinahitaji nishati ya umeme hivyo imefika hatua ambayo
masuala ya nishati ni muhimu yakapewa nafasi katika vikao hivyo vya
maendeleo kwa kuwa ikiwa haitapewa nafasi inaweza kuchangia kupUnguza
kasi ya maendeleo tarajiwa.
Aidha, akizungumza kwa nyakati
tofauti katika mikutano ya hadhara katika vijiji vya Itwangi na Nyambui,
Mgalu amesisitiza kuhusu Wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo
kuhakikisha kuwa wanaripoti katika ofisi za Serikali kuanzia ngazi za
Vijiji, Wilaya na Mikoa ili kuweka mazingira bora na rafiki ya
utekelezaji ka wa miradi husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Zainabu Taleck, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
mkoani humo kuwasilikiza wateja na kuhakikisha linasambaza nishati hiyo
kwa wananchi wengi zaidi ikizingatia kuwa, mahitaji ya umeme hususani
maeneo ya mijini yamekuwa makubwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
Josphine Matiro aliiomba wizara kuwafikiria wananchi ambao wako tayari
kuchangia ili kupata huduma ya nishati hususan kwa walio katika maeneo
ya pembezoni.
Naye Msimamizi wa Mradi wa REA
Hussein Shemdasi, amewataka wananchi watakaounganishwa na huduma ya
umeme kuutumia kwa uzalishaji ili kujiongezea kipato. Pia, alisisitiza
kuhusu wakandarasi kushirikiana na viongozi wa Serikali ili kuwezesha
mradi huo kutekelezwa kikamilifu.
Kwa upande wake, Meneja wa Tanesco
Kanda ya Magharibi Macline Mbonile aliwataka wananchi kufanya
maandalizi kipindi cha mradi ili wanapofikiwa wakati wa utekelezaji
waweze kuunganishwa na huduma hiyo.
Post a Comment