ZOEZI LA UHAKIKI WA VIWANJA MBEYA YAINGIA DOSARI
MBEYA
ZOEZI la uhakiki na
utambuzi wa Viwanja vya wakazi wa Mtaaa wa Sisitila, kata ya Iyunga jijini
Mbeya limeingia dosari baada ya kulalamikiwa na wananchi kuwa zoezi hilo linatekelezwa
kinyume na Maagizo ya Serikali ya Mkoa.
Mwishoni mwa mwaka
jana Mkuu wa Mkuu wa Mbeya Amos Makalla aliiagiza halamshauri ya jiji la Mbeya
kutowaondoa wananchi ambao hawakulipwa fidia na ambao maeneo yao
hawakufanyiwa tathmini kuwaacha wabaki katika maeneo yao ya asili.
Hata hivyo Aliagiza
kufanyika Mchakato wa haraka kwa ajili ya kuwalipa ongezeko la Mapunjo ya zaidi
ya sh.milioni 800 watu ambao hawakulipwa fidia wakati wa mradi wa kuwahamisha
kwa ajili ya kupima viwanja hivyo.
Wakizungumza na Diratz news kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa mtaa huo walisema wataalamu
kwa kushirikiana na kamati ilyoundwa wananchi wamekuwa wakiwatoza baadhi ya
wananchi kiasi cha sh.50,000, kwa ajili ya kupima maneo yao.
“Mkuu wa Mkoa
alitoa Maagizo kwamba watupimie maeneo yetu ya asili tuendelee kibaki lakini
tunachokiona ni ujeuri kwani wanakuja kutambua maeneo yetu lakini
wanatuzoza fedha, na kama huna fedha hawakuoneshi eneo lako au wanakwambia
limekwishauza,” alisema Dicksoni John.
Karibu Asajile,
alisema agizo la Mkuu wa mkoa kurudisha maeneo ya asili ya wakazi wa Mtaa wa
Sisitila linawahusu wale ambao hawajalipwa fedha za fidia na halmashauri.
Alisema
kinachowashangaza baadhi ya wananchi ni kuwa wanapokuwa wanapimiwa maeneo yao
ya sili wanapewa eneo dogo ukilinganisha na lilivyokuwa awali huku sehemu
nyingine zikikatwa na kupewa watu wengine.
“Ndugu Mwandishi wa
Habari Mgogoro Mkubwa unaojitokeza ni kwamba Mkuu wa Mkoa alisema ambao
hatujalipwa turudishiwe maeneo yetu lakini unakuta baada ya kupimwa maeneo hayo
tunaambulia eneo dogo tofauti na mwanzo yani unaweza kutegemea kiwanja
vinne lakini ukaambulia kimoja na ukilalamika hausikilizwi,”alisema
Gastoni Mwangisi
alisema alitozwa kiasi cha Sh. 50,000 na watu wanaoendesha zoezi la utambuli
bila kukatiwa risiti ya malipo huku wakimweleza fedha hiyo ni kwa ajili ya
kulipia gharama za utambuzi wa eneo lake.
Mjumbe wa Serikali
ya Mtaa huo Thabit Nzunda alisema anafuatilia suala hilo kwa ukaribu katika
mamlaka husika ili hatua stahiki ziweze kuchukiliwa.
Afisa ardhi wa jiji
la Mbeya Patriki Mwakilili alikiri kuwa Tume ya wataalamu inaendesha zoezi la
uhakiki na utambuzi wa maeneo katika mtaa huo ili kuhakikisha kila mwananchi
anapata eneo lake stahiki.
Kuhusiana na
wananchi kutozwa kiasi cha 50,000 kwa ajili ya vipimo alisema ofisi yake haina
taarifa hivyo atafuatilia ili aweze kupata maelezo ya kina na amewataka watu
waliotozwa fedha hizo wafike ofisini kwake.
Akizungumzia
Mapunjo ya Fidia alisema halmashauri imefungua akaunti ya Maalum kwa ajili ya
kuwalipa fedha watu ambao wamefanyiwa uhakiki na kwamba zoezi la fidia litaanza
kufanyika mara moja mara baada ya kukamilisha taratibu zote.
Post a Comment