Header Ads


ILEJE YAANZA MAANDALIZI YA MBIO ZA MWENGE 2018




Mkuu wa Wilaya Mhe.Joseph Mkude(kulia) akizungumza kwenye kikao hicho,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Haji Mnasi.


ILEJE-SONGWE
Zikiwa zimebaki siku chache ili kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru huko mkoani Geita, wilaya ya Ileje iliyopo mkoani Songwe imeanza maandalizi ya kuupokea na kuukimbiza mwengehuo.
Ikiwa kinara wa mbio hizo kwa mkoa wa Songwe hapo mwaka jana kwa kuzipiku halmashauri nne wilaya hiyo imeshaanza vikao vya maandalizi ilikuweza kujiweka katika nafasi nzuri kitaifa na kikanda kwa mwaka 2018.

Akisoma taarifa kwenye kikao cha maandalizi,Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo.Ndugu Bakari Nikata aliwaeleza wajumbe hao kuwa,wilaya ya Ileje iliweza kushika nafasi ya kwanza kimkoa,huku ikiwa ya 39 kikanda na ikisimama nafasi ya 167 kitaifa kati ya Halmashauri 195.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya Mhe,Joseph Mkude aliwataka kutoridhishwa na
matokeo ya mwaka jana kwa kuwa kinara kimkoa kwani Halmashauri zilizofanya vibaya lazima zimejipanga ili kuepukana na nafasizilizo kuwepo na kuu kwamua mkoa kwenye nafasi ya pili toka mwisho kwakushika nafasi ya 30 kati ya mikoa 31.


Aidha,aliwataka wananchi kwa ujumla kuungana pamoja katika shughuli za kitaifa ikiwani,Njia mojawapo ya uzalendo kwaTaifa bila kujali itikadi za kisiasa,dini au ukabila.
Naye,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mhe.Ubatizo Songa alitaka wajumbe kupanga kuu kimbiza Mwenge katika kanda zoteili wananchi wote waweze kupata fursa ya kushiriki katika matukio ya kitaifa.

Viongozi wa dini ambao wamekuwa wajumbe wa vikao hivyo waliomba miradi inayo pitiwa na Mwenge iwe endelevu na inayoleta mabadiliko chanya katika jamii.
Padri Didas Chauwele kutoka Parokia ya Mt.Mbagatuzinde ya Itumba aliwashauri viongozi wa serikali kushikamana ili kuweza kufikia malengo na maamuzi ya vikao hivyo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka jana aliipongeza wilaya ya Ileje kwa mshikamano uliokuwepo kwa Serikali Kuu,Halmashauri,Vyama vya Siasa viongozi wa Dini pamoja na wananchi kwa ujumla yakiwemo matangazo ya mubashara kwa Halmashauri zote za mkoa wa Songwe.

No comments

Powered by Blogger.