MKUU WA WILAYA YA KYELA AWATAKA WANAFUNZI KUTOKUFIKIRIA KUOA AU KUOLEWA
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta |
KYELA-MBEYA
MKUU
wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya Claudia Kita, amewataka wanafunzi
ambao hawajachaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka huu kuachana na Fikra
za kutaka kuoa au kuolewa na badala yake wafikirie kujiunga na elimu ya ufundi
stadi ili wajikwamue kiuchumi.
Kita
ametoa rai hiyo jana wakati akizungumza na Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya
Kyela walipokuwa kwenye kikao cha kujadili na kupitia taarifa za kamati
mbalimbali katika kipindi cha robo mwaka fedha 2017/2018.
Mkuu
huyo wa Wilaya alisema Jumla ya wanafunzi 2710 kati ya 7338 waliofanya mitihani
ya kumaliza elimu ya msingi hawajabahatika kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha
kwanza kutokana na kufanya Vibaya.
Alisema
Idadi hiyo ya wanafunzi waliosalia nyumbani ni kubwa hivyo wazazi na walezi
wana wajibu wa kuhakikisha wanawapeleka kwenye shule binafsi au shule za
ufundi ili wawezi kupata ujuzi wa kufanya kazi za Mikono utakaofanya waweze
kujitegemea hapo baadae.
“kwa
takwimu nilizonazo wanafunzi 2710 hawajachaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza
mwaka huu hao wapo nyumbani, nitoe rai kwa wazazi na walezi tusiwaacha
tuwapeleke shule za ufundi wakajifunze kazi za mikono, pia wao waachanae na
fikra za kuoa au kuolewa kwa kuwa bado wana umri mdogo,”
“Pia
na nyie Madiwani mtusaidie katika hili nah ii itasaidia hata vijana wetu ambao
wapo nyumbani kutojiingiza kwenye Makundi Mabaya ikiwemo Madawa ya Kulevya na
uhalifu mwingine kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira,” alisema.
Aidha,
Mkuu huyo wa wa wilaya aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuendelea na kilimo
katika msimu huu na kuwahakikishia kuwa Mbolea aina ya UREA ipo ya
kutosha isipokuwa bei imeongezeka kidogo kutokana na gharama za manunuzi
na usafirishaji.
Hata
hivyo hakuweka bayana gharama ya sasa ya Mbolea hiyo kwa madai kuwa hadi kamati
ya Pembejeo ya wilaya itakapoketi kupitia mchakato mzima wa usambazaji na
kusisitiza kuwa inapatikana kwa bei ambayo kila mkulima anaweza kuimudu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya hiyo Hunter Mwakifuna aliwataka
Madiwani na wananchi kutotafsri vibaya kauli ya rais John Magufuli ya
kupiga marufuku michango shuleni.
Alisema
Kauli ya raisi inawapiga marufuku walimu na maafisa elimu kuwatoza michango
wazazi na walezi na kwamba wananchi wanaweza kuamua kuchangia michango mbalimbali
ikiwemo chakula kwa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri.
Post a Comment