Header Ads


BMT YATANGAZA KAMATI ITAKAYO SIMAMIA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA

Mohamed Kiganja-Katibu Baraza la Michezo Tanzania


Katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa BMT Mohamed Kiganja ametangaza kamati maalum itakayosimamia mchezo wa ngumi za kulipwa ikiwa ni ahadi iliyotolewa na waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Harrison Mwakyembe wakati akipokea rasimu ya katiba Februari 03.

Kiganja ametangaza majina ya kamati hiyo hukua kieleza kwa kina namna itakavyokua ikifanya kazi kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa.


Wakati huo huo Kiganja amewataka wadau wa michezo nchini kufuata utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yao kwa lengo la kutatua migogoro inayoibuka kwa pande mbili ambazo huibuka mara kwa mara.

Kiganja ametangaza hatua ya kufuatwa kwa utaratibu huo baada ya badhi ya wadau kushindwa kuziheshimu katiba zao pamoja na kutotambua mpangangilio wa kuwasilisha malalamiko hadi kufikia kwa waziri mwenye dhamana.

No comments

Powered by Blogger.