TFF YAPANGA RATIBA YA 16 BORA MICHUANOM YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP
Shirikisho la soka nchini TFF kwa kushirikiana na
wadhamini wakuu wa kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) hapo jana jioni
limepanga ratiba ya 16 bora ya michuano hiyo kwa kuzishirikisha timu 16 zilizofuzu
kucheza hatua hiyo.
Shughuli za kupanga ratiba ya hatua hiyo ya 16
zimefanyika mapema hii leo kwenye studio za Azam TV na kurushwa mubashara kwa
lengo la mashabiki wa soka wote nchini kushuhudia jambo hilo likifanyika kwa
uwazi.
Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans
wamepangw akukutana na Majimaji FC ambao watakua nyumbani katika uwanja wa
Majimaji.
Mbali na Young Africans kwenda Songea, vigogo
wengine Azam FC watamenyana na KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam, wakati
mkoa wa Shinyanga utahodhi mechi mbili mfululizo, kwanza ni Stand United na
Dodoma FC na baadaye Buseresere na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kahama.
Michezo mingine ya hatua ya 16 bora ya kombe la
shirikisho JKT Tanzania watakuwa wenyeji Ndanda FC Uwanja wa Mbweni, Dar es
Salaam, Kiluvya United na Tanzania Prisons Uwanja wa Filbert Bayi, Kibaha,
Pwani, Singida United na Polisi Tanzania Uwanja wa Namfua na Njombe Mji dhidi
ya Mbao FC Uwanja wa Saba Saba, Njombe.
Mara baada ya kukamilika kwa shughuli ya kupangwa
kwa ratiba hiyo, tulipata nafasi ya kuzungumza na meneja wa Azam FC Philip
Alando na kumuuliz anamna walivyopokea hatua ya kupangwa na KMC.
Naye meneja wa KMC Kalambo Kalambo amesema wamepangwa na timu bora na wanaamini mpambano wao utakua na ubora wa hali ya juu.
Michezo yote ya hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zitafanyika kati ya Februari 22 na 25.
Post a Comment