UONGOZI WA TIMU YA KINONDONI MUNICIPAL COUNCIL YATOA NENO KWA MARA YA KWANZA
Uongozi wa klabu ya Kinondoni Municipal Council (KMC)
kwa mara ya kwanza umetoa kauli baada ya kiksoi cha klabu hiyo kufanikiwa kupata
nafasi ya kucheza michuano ya ligi ligi kuu ya soka Tanzania bara, ikitokea
ligi daraja la kwanza msimu huu wa 2017/18.
Kikosi cha Kinondoni Municipal Council kilipata
nafasi hiyo mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuibuka na ushindi katika
mchezo wao wa mwisho wa kundi B, kwa kuifunga JKT Mlale mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mstahiki meya wa manispaa ya Kinondoni Bnjamin
Sitta amesema ni furaha kubwa sana kwa upande wao kama viongozi wa manispaa
hiyo kwa kufanikisha suala la kuwa na timu katika ligi kuu ya soka Tanzania
bara.
Sitta amesema wameandaa tukio maalum kwa
kuipongeza timu yao kwa kuwashirikisha viongozi wa wilaya ya Kinondoni pamoja
na wananchi wa wilaya hiyo.
Sitta pia akaeleza mipango ya baadae ya klabu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) baada ya kufanikisha lengo la kupanda daraja la kucheza ligi kuu.
Naye kocha mkuu wa KMC Fred Felix Minziro amesema
anakiamini sana kikosi chake na hana mpango wa kukipangua utakapofika wakati wa
usajili wa kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Minziro amesema hana mpango wa kuwafikiria sana
wachezaji wa kimataifa ambao wamekua wakipewa kpaumbele katika baadhi ya klabu
za soka hapa nchini, na badala yake ataangalia uwezo wa mchezaji kwanza na
kisha kutoa idhini asajiliwe.
Post a Comment