KLABU YA SIMBA YAJIAANDAA NA MAANDALIZI YA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO
Klabu ya SImba imetangaza sehemu ya maandalizi ya
mchezo wake wa kwanza wa kimataifa wa michuano ya kombe la shirikisho kwa mwaka
huu 2018 ambao utawakutanisha dhidi ya Gendarmerie Tnale kutoka nchini Djibout.
Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara
ametangaza sehemu ya maandalizi ya mchezo huo ambao utafanyika mwishoni mwa
juma hili kwenye uwanja wa taifa, katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Manara amesemataratibu za awali za mchezo huo
zimeshakamilishwa baada ya kupokea taarifa za ujio wa wapinzani wao kutoka
nchini Djibout pamoja na waamuzi watakaochezesha mpambano huo kutoka nchini
Sudan kusini.
Katika hatua nyingine Haji Manara ametoa wito kwa mashabii wa klabu ya Simba kujenga tabia ya kuacha kuwazomea wapinzani wao wanapokua katika michuano ya kimataifa, ili kujenga hadhi ya uungwana katika mchezo wa soka ambao kwa Tanzania unahitaji msaada wa matokeo mazuri.ka ki
Manara amesema ombi hilo limkatiezingatia suala la
uzalendo ambao siku zote umekua ukipigiwa kelele katika kila sekta hapa nchini.
Post a Comment