WATUMISHI WOTE WA SEREKALI WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE WAMEPEWA SIKU 30 WAWE WAMEHAMIA KWENYE VITUO VYAO VYA KAZI
Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa
jimbo la vwawa japhet ngailonga hasunga wakati wa ziara yake katika kata ya
kilimapimbi tarafa alipo kuwa akisikiliza kero za wananchi ambapo
amewataka watumishi wote wa serikali wahamie sehemu zao za kazi kwani
imeonekana watumishi wengi wanaishi mjini na kwenda kufanya kazi vijijini.
Mh hasunga ameongeza kuwa mtumishi
yeyote ambaye hatakaa eneo lake la kazi sheria itachukua mkondo wake hivyo
ndani ya siku 30 wawe wamehamia sehaem zao za kazi.
Mmoja wa watumishi wa serikali
wilayani mbozi christabell mapundamwalimu mkuu shule ya msingi ikomela amekili
kuto kaa eneo la kazi ambapo amesema kuwa changamoto kubwa ni miundombinu
ambayo si rafiki kwao lakini pia baadhi ya watumishi wamehamishwa maeneo yao ya
kazi bila kuwapa usafili kwa ajili ya kusafilishia mizigo yao.
Afisa tarafa wa vwawa haji hamisi
Ibrahim amekili kuwa watumishi wengi hawakai maeneo yao ya kazi kwani hata
watumishi wa kata wengi hawakai maeneo yao ya kazi hivyo inakuwa ngumu
kuwaambia watumishi wa ngazi ya kijiji wakati wao wenyewe hawakai maeneo yao ya
kazi hivyo wametoa siku 30 wote wawe maeneo yao ya kazi.
Baadhi ya wanachi Sophia
joseph na aziza mgala wameshukuru kwa hatua iliyochukuliwa na serikali kwani
huwa inapotokea dharula inakuwa ngumu kutatuliwa kwa wakati..
Post a Comment