Header Ads


KAMPUNI YA STARTIMES YAMWAGA PESA KWENYE MCHEZO WA KIKAPU





Uongozi wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam BD umeingia mkataba na kampuni ya Star Times kwa ajili ya kuendesha hatua ya mtoano ya ligi ya mkoa huo ambayo itaanza baadae mwezi huu.

Mkurugenzi wa ligi mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam RBA Peter Mpangala amesema wanaamini udhamini walioingia hii leo, watafanikisha lengo la kuwa na michuano mizuri na yenye ushindani mkubwa.

Naye afisa uhusiano wa kampuni ya Star Times Samwel Gisay ameweka hadharani mipango mikakati ambayo wameifanya hadi kufikia hatua ya kuingia mkataba na uongozi wa chama cha mchezo wa mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam.

Wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam okare Omesu ametoa shukurani zake za dhati kwa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia ofisi ya mkurugenzi wa maendeleo ya michezo.

No comments

Powered by Blogger.