UONGOZI WA SIMBA WAKEMEA MABADILIKO YA KATIBA
Mwenyekiti
wa bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba Khamis Kilomoni ametoa tamko la kukemea
mchakato wa mabadiliko unaotarajiwa kufanyiwa mchakato kupitia mkutano mkuu wa
dharura wa wanachama ulioitishwa August 13 mwaka huu.
Akiwa na baadhi ya wanachama wanaounga mkono itikadi za kukataa
mfumo wa mabadiliko ya kiuongozi ndani ya klabu hiyo, Kilomoni amesema uongozi
wa kladbu ya Simba pamoja na Mohamed Dewji ambaye amedhamiria kuiendesha klabu
hiyo kw amfumo wa jhisa wanajua nini ambacho amewaagiza ili kukamilisha mpango
huo.
Kilomoni amesema kama maagizo yake yatashindwa kufanyiwa kazi
kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba, hakuna jambo lolote
litakalopita kuputia mkutano wa dharura wa wanachama utakaofanyika baadae mwezi
huu.
Naye katibu mkuu wa bodi ya wadhamini ya klabu ya Simba Damle
Khamis Fikirini Mkwabi akaongezea jambo juu ya maneno yaliyozungumzwa na
mwenyekiti wake Khamis Kilomoni.
Post a Comment